Waziri wa Biashara na maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe Omar Said Shaaban akizungumza wakati akifunga mkutano wa wakuu wa Taasisi za SMZ na SMT katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi huko kituo cha maonesho ya biashara nyamazi Zanzibar.
Mwenyekiti wa jukwaa la Taasisi za SMZ na SMT (CEOs) Latifa M.Khamis akisoma maazimio wakati wa kufunga mkutano wa wakuu wa Taasisi hizo uliofanyika katika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi Nyamanzi katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya viongozi wa TAASISI za SMT na SMZ wakiwa katika Mkutano wa wakuu wa TAASISI hizo uliojadili tija zilizopatikana ndani ya Taasisi hizo katika kipindi cha miaka 60 ya Mapinduzi,hafla iliyofanyika Ukumbi wa dkt.Hussein Mwinyi Nyamanzi Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO ZANZIBAR
Na Rahma Khamis Maelezo
Waziri wa Biashara na maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe Omar Said Shaaban amesema Wizara ipo tayari kutoa mashirikiano kwa wafanya biashara ili kukuza pato la taifa.
Akizungumza wakati akifunga mkutano wa watendaji wakuu wa SMT na SMZ katika Ukumbi wa Dkt Mwinyi Nyamanzi amesema utayari huo unahusisha na utoaji wa vibali kwa wafanya biashara ili kuendeleza biashara zao.
Mhe Shaaban pia amewaomba watendaji wa Taasisi za SMZ na SMT kuzingatia mipango madhubuti waliyojiwekea ili kufikia malengo waliyoyakusudiwa.
Aidha amezishukuru Taasisi, Mashirika na Wadau mbalimbali kwa kuwaunga mkono na kufanikisha kufanyika mkutano huo.
Aidha aliendelea kusisistiza taasisi za Serikali kuutumia Ukumbi wa mikutano wa Dkt Hussein Mwinyi uliopo katika kituo cha Manyesho ya Biashara Nyamazi kwa kufanya shughuli zao mbalimbali ili kuongeza pato la taifa.
Akiwasilisha maazimio ya mkutano huo Mwenyekiti wa Jukwaa la Taasisi hizo Latifa Khamis amesema Jukwaa la viongozi wa Mashirika na Taasisi za Umma kutoka SMZ kudhamiria kukamilisha usajili rasmi ifikapo robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Ameongeza kuwa Jukwaa hilo limedhamiria kutoa ushirikiano wa kiutendaji kwa Jukwaa tarajiwa la Watendaji Wakuu la SMZ katika zoezi la kurasimisha Jukwaa hilo kupitia usajili rasmi.
Aidha amefahamisha kuwa Wakurugenzi Wakuu wote kwa umoja wao na kwaniaba ya Mashirika wanayoyaongoza wanaahidi kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo ya Taasisi na dhamira ya waheshimiwa ,Marais na Serikali zote mbili kuchochea utoaji wa huduma katika Taasisi hizo.
Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za SMZ na SMT ulifunguliwa January 13 na Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Axaud Kigahe Katika kuseherehekea miaka 60 ya Mapinduzi