NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe.Patrobas Katambi,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe.Patrobas Katambi,amesema Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Wanachama wa TALGWU katika maeneo yao ya kazi katika kusimamia utekelezaji wa maendeleo ya nchini.
Mhe.Katambi ameyasema hayo leo Januari 15,2024 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU).
Katambi ,amesema Serikali itaendelea kulinda na kuendeleza haki za wafanyakazi nchini huku ikitambua, kuheshimu na kuuenzi mchango wa Watumishi wa Umma ambao ni Wanachama TALGWU.
“Waajiri kuhakikisha wanafuata matakwa ya sheria za kazi za nchi na kudumisha mahusiano mema kazini kwa manufaa yenu wenyewe na wafanyakazi wenu na Utashi wa Serikali katika kutekeleza wajibu wake wa kulinda haki za wafanyakazi nchini umejidhihirisha wazi kupitia hatua za kisheria na za kiuchumi ambazo imekuwa inatekeleza,”
Na kuongeza kuwa”Tunatambua kuwa wengi wenu mnafanya kazi katika mazingira magumu lakini Serikali haitachoka kuzifanyia kazi kero na changamoto zenu na kutafuta njia mbalimbali za kuzipatia ufumbuzi sambamba na kuendelea kuboresha mazingira ya kazi,”amesema Katambi
Kuhusu Changamoto Mhe.Katambi,amewahakikishia TALGWU kuwa Serikali ipo tayari kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha wafanyakazi wanatekeleza majukumu yao kwa amani huku changamoto walizonazo zikiwa zinapatiwa ufumbuzi na Serikali chini ya uongozi madhubuti wa Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Aidha amewataka wanachama wote wa TALGWU kutambua kuwa ulinzi wa haki za wafanyakazi huanzia kwa wao wenyewe kwa kuzingatia dhana ya haki ba wajibu hivyo chana hicho kinapasawa kuwakumbusha wafanyakazi kujiepusha na vitendo vinavyoendekea kinyume na misingi na maadili ya utumishi wa umma.
“Wafanyakazi kama hawatajiepusha na matendo hayo maovu basi watafanya kazi ya kutetea na kulinda haki zao kuwa ngumu kwao na wadau wengine kama sisi. Lazima wakati wote tukumbuke kuwa kudai haki kunaenda sambamba na kutimiza wajibu,”amesisitiza Katambi
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TALGWU Taifa Bw.Tumaini Nyamhokya amesema kuwa kuna kilio Kikubwa cha wafanyakazi walio na elimu ya darasa la Saba ambao mishahara yao kati ya miezi mitatu hadi sita haikulipwa ,zile siyo fedha za hisani ni mishahara yao lakini pia na hata walivyosimama walisimama kimakosa kwani hata barua zao tunazo.
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe.Patrobas Katambi,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe.Patrobas Katambi,akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa TALGWU Taifa Bw.Tumaini Nyamhokya,akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Ndg. Rashid Mtima,akitoa taarifa ya Kikao cha Baraza Kuu TALGWU Taifa kilichofanyika leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.
BAADHI ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe.Patrobas Katambi (hayupo pichani), wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.