Naibu waziri wa Viwanda na Biashara WA Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania Exaud Kigahe akizungumza wakati akifungua mkutano wa wakuu wa Taasisi za SMZ na SMT katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi,Hafla iliyofanyika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi kituo cha maonesho ya Biashara nyamazi Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Na Rahma Khamis Maelezo
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Exaud Kigahe amezitaka Taasisi zinazohusika na Biashara kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi ili kujenga uwelewa juu ya biashara.
“Sisi wa Tanzania tunategemea biashara hivyo tujitahidi kufahamu umuhimu wa biashara na tuondoe malalamiko” alisisitiza.,Naibu Waziri wa
Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Dkt Mwinyi Nyamanzi Wilaya Magharib B’ katika ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za SMT na SMZ katika kusheherekea miaka 60 ya Mapinduzi.
Amesema wafanya biashaa wengi hawana uwelewa juu ya makato na tozo za biashara kati ya Zanzibar na Tanzania jambo linalopelekea malalamiko hivyo ipo haja kwa taasisi husika kuendelea kutoa elimu ya kuwajengea uelewa dhidi ya malalamiko hayo.
Aidha amefahamisha kuwa kuna changamoto nyingi katika Taasisi za biashara hivyo ni vyema kukaa pamoja nakushirikiana kuzitatua changamoto hizo ili kutoa fursa kwa wafanya biashara kuendelea na biashara zao pamoja na kuleta maendeleo.
Ameeleza kuwa ikiwa wanakaribia kufikia miaka 60 ya Muungano wa Tanzania amezitaka Taasisi husika Kuwasaidia Sekta Binafsi ili kuweza kutoa mchango wao katika biashara.
“Sisi tuna haja ya kusimamia na kutekekeza malengo ya biashara ili kuleta mafanikio yetu katika muungano wetu” alisema
Ameongeza kuwa Tanzania Bara na Zanzibar ni nchi moja hivyo ni vyema kushirikiana kwa pamoja ili kuleta mafanikio kwa pande zote mbili.
Aidha amewashukuru Marais wa Serikali zote mbili kwa kazi kubwa wanazozifanya ya kuleta maendeleo nchini.
Nae Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe Rashid Salim amesema kuwa kikao hicho kitasaidia kujenga mashirikiano zaidi, kujifunza pamoja na kubadilishana uzoefu.
Aidha ameeleza kuwa kikao hicho pia kitatoa fursa kwa watendaji wa Taasisi hizo kufikia malengo katika utendaji wa kazi zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wakuu wa Taasisi Latifa Khamis amefahamisha kuwa jukwaa hilo limeanza mwaka 2016 kwa lengo la kukuza ushirikiano ili kupanua ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Amesema kuwa kikao hicho kina lengo la kutekekeza malengo ya miaka 60 ya Mapinduzi ambayo yana mafanikio makubwa .
Aidha amefahamisha kuwa tangu kuanzishwa kwa jukwaa hilo wamefanikiwa kubadilishana uzoefu na kukubaliana katika mambo mbali mbali ya kuimarisha utendaji wa majukumu yao.
Nao washiriki wa mkutano huo wamesema kuwa wataendelea kushirikiana baina yao kwa kufanya kazi kwa pamoja ili kufikia malengo yayaliyokusudiwa.
Katika Makutano huo Taasisi mbali mbali za SMZ na SMT zilishiriki ikiwemo TANESCO, TRA, ATC, TPA, LATRA na TASAC.
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara WA Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania Exaud Kigahe akicheza Ngoma ya kibati pamoja na wasanii wa Ngoma hiyo kutoka Chuo cha mafunzo wakati alipofika kufungua mkutano wa wakuu wa TAASISI za SMT na SMZ uliojadili mchango na mafanikio ya Taasisi hizo katika miaka 60 ya Mapinduzi ,Hafla iliyofanyika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi eneo la maenesho ya Biashara nyamazi Zanzibar
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara WA Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania Exaud Kigahe akipokelewa kwa Ngoma ya kibati kutoka kwa wasanii wa Chuo cha mafunzo wakati alipofika kufungua mkutano wa wakuu wa TAASISI za SMT na SMZ uliojadili mchango na mafanikio ya Taasisi hizo katika miaka 60 ya Mapinduzi ,Hafla iliyofanyika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi eneo la maenesho ya Biashara nyamazi Zanzibar
Mwenyekiti wa jukwaa la Taasisi za SMZ na SMT (CEOs) Latifa M.Khamis akitoa maelezo mafupi kuhusiana na umoja huo katika mkutano wa wakuu wa Taasisi hizo uliofanyika katika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi Nyamanzi katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Naibu katibu mkuu Wizara ya biashara na maendeleo ya Viwanda Zanzibar Rashid A. Salim akimkaribisha Naibu waziri wa Viwanda na Biashara WA Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania Exaud Kigahe kifungua mkutano wa wakuu wa Taasisi za SMZ na SMT katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi huko Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi eneo la maenesho ya Biashara nyamazi Zanzibar.
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara WA Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania Exaud Kigahe akizungumza wakati akifungua mkutano wa wakuu wa Taasisi za SMZ na SMT katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi,Hafla iliyofanyika Ukumbi wa Dkt Hussein Mwinyi kituo cha maonesho ya Biashara nyamazi Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR