*Ndugu wananchi wenzangu* wa Jimbo la Singida Mashariki nachukua fursa hii kuwatakia *Kheri ya Mwaka Mpya 2024*.*Namwomba Mwenyezi Mungu awape Baraka, Afya Njema na Neema katika mwaka huu 2024*.
*Ndugu wananchi wenzangu* baada ya salamu za Mwaka Mpya napenda kuwafahamisha kuwa Kamati ya Mfuko wa Jimbo (*Mfuko wa Mbunge*) ambayo *Mwenyekiti ni Mbunge iliyoketi tarehe 04.01. 2024* iliweza kujadili maombi ya miradi ya wananchi kutoka *Kata Kumi na tatu( 13)* na baada ya kikao kamati ilitenga fedha kiasi cha *Sh 67,498,970* katika miradi hiyo kwa mchanganuo kama ifuatavyo;
1. Pesa kwa ajili ya *Kusaidia ujenzi wa vyoo vya shule ya Msingi ya Sambaru katika Kata ya Mang’onyi,Kijiji cha Sambaru kiasi cha Sh 2,000,000*.
2. Pesa kwa ajili ya *Kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa matundu ya vyoo Shule ..ya msingi Mwau Kata ya Mang’onyi,Kijiji cha Mwau kiasi cha Sh 2,000,000*.
3. Pesa kwa ajili ya *Kusaidia umaliziaji wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu Shule ya Msingi Choda Kata ya Mkiwa,Kijiji cha Choda kiasi cha Sh 2,000,000*.
4. Pesa kwa ajili ya *Ujenzi wa Kituo cha Polisi Kata ya Mkiwa,Kijiji cha Mkiwa Sh 5,000,000*.
5. Pesa kwa ajili ya *Ujenzi wa matundu ya vyoo Shule ya Sekondari Mkunguwakihendo Kata ya Kikio Kiasi Sh 2,000,000*.
6. Pesa kwa ajili ya *Kusaidia ujenzi wa madarasa Shule Shikizi ya Mwitumi Kata ya Kikio,Kijiji cha Nkundi kiasi cha Sh 10,000,000*.
7. Pesa kwa ajili ya *Kusaidia ujenzi wa Shule ya Utayari katika shule shikizi ya Kinyaghimbi Kata ya Ikungi Kijiji cha Matongo kiasi cha Sh 3,000,000*.
8. Pesa kwa ajili ya *Ununuzi wa samani za ofisi Shule ya Msingi Mbughantigha Kata ya Ikungi,Kijiji cha Matongo kiasi cha Sh 1,000,000*.
9. Pesa kwa ajili ya *Ununuzi wa mashine ya kudurufu (Photocopy Machine),Shule ya Msingi Matongo Kata ya Ikungi katika Kijiji cha Matongo kiasi cha Sh 3,000,000*.
10. Pesa kwa ajili ya *Ununuzi wa Printer Shule ya Sekondari Matongo Kata ya Ikungi ,Kijiji cha Matongo kiasi cha Sh 1,000,000*.
11 .Pesa kwa ajili ya *Umaliziaji wa darasa na ukarabati wa kisima cha maji Shule ya Msingi Tumaini Kata ya Issuna,Kijiji cha Tumaini kiasi Sh 2,000,000*.
12. Pesa kwa ajili ya *Kusaidia ujenzi wa madarasa Shule Shikizi Muve Kata ya Mungaa,Kijiji cha Kinku kiasi cha Sh 5,000,000*.
13.Pesa kwa ajili ya *Kusaidia ujenzi wa matundu ya vyoo Shule ya Msingi Kimbwi Kata ya Makiungu,Kijiji cha Kimbwi kiasi cha Sh 1,500,000*.
14.Pesa kwa ajili ya * Kusaidia ujenzi wa madarasa *Shule ya Msingi King’inga Kata ya Unyahati,Kijiji cha Ulyampiti kiasi cha Sh 1,500,000*.
15.Pesa kwa ajili ya * Kusaidia ukarabati wa vyumba vya madarasa 2 na choo cha wanafunzi *Shule ya Msingi Kinyamwandyo Kata ya Unyahati,Kijiji cha Kinyamwandyo kiasi cha Sh 2,000,000*.
16.Pesa kwa ajili ya *Kusaidia ujenzi wa matundu ya vyoo katika Zahanati Kata ya Dung’unyi, Kijiji cha Samaka kiasi cha Sh 1,500,000*.
17.Pesa kwa ajili ya * Kukarabati Ofisi ya *Mtendaji wa Kata ya Siuyu,Kijiji cha Siuyu kiasi cha Sh 3,000,000*.
18.Pesa kwa ajili ya * Kusaidia ujenzi wa madarasa 2 *Shule Shikizi ya Msui Kata ya Misughaa,Kijiji cha Msule kiasi cha Sh 2,000,000*.
19.Pesa kwa ajili ya * Kusaidia ujenzi wa *Zahanati Kata ya Ntuntu,Kijiji cha Mampando kiasi cha Sh 1,498,970*.
20.Pesa kwa ajili ya * Kusaidia ujenzi wa madarasa *Shule Shikizi ya Sanya Kata ya Lighwa,Kijiji cha Lighwa Kiasi cha Sh 3,000,000*.
21.Pesa kwa ajili ya *Kusaidia ujenzi wa maabara Shule ya Sekondari ya Lighwa Kata ya Lighwa,Kijiji cha Mwisi Kiasi cha Sh 2,000,000*.
22.Pesa kwa ajili ya * Kusaidia umaliziaji wa nyumba za walimu *Shule ya Msingi Ntewa A Kata ya Ntuntu,Kijiji cha Ntewa A kiasi cha sh 2,000,000*.
23.Pesa kwa ajili ya * Kusaidia ujenzi wa madarasa 2 *Shule Shikizi Ititimo Kata ya Issuna,Kijiji cha Issuna A Kiasi cha Sh 2,000,000*.
24. Pesa kwa ajili ya * Kusaidia ujenzi wa madarasa *Shule Shikizi Mlumbi Katanya Ntuntu,Kijiji cha Ntewa A Kiasi cha Sh 2,000,000*.
25.Pesa kwa ajili ya * Kusaidia ujenzi wa maabara *Shule ya Sekondari Mang’onyi Shanta Kata ya Mang’onyi,Kijiji cha Tupendane Kiasi cha *Sh 4,000,000*.
Kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki, Tunamshukuru sana *Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, *Mhe. Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini* kwa kuendelea kuboresha maisha yetu Wana Singida Mashariki kwa kuendelea kutuletea miradi mikubwa ya maendeleo na kushughulikia changamoto za wananchi katika wilaya yetu. *Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020- 2025 inaendelea kutekelezwa.*
*Ndugu wananchi wenzangu* wa Singida Mashariki tunayo kila sababu ya kutoa shukuran kwa *Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan* kwa kuendelea kutupa fedha nyingi kwa ajili ya kutatua miradi ya Maendeleo. Tumuombee *Mhe. Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan* Mwenyezi Mungu ampe Afya Njema na kumlinda vyema ili aendelee na maono yake mazuri katika Kujenga Taifa Letu.
*Mhe. Rais wetu Mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan* ameendelea kusikia kilio chetu kupitia sauti yenu Bungeni.
*Ndugu wananchi wenzangu* kwa dhati kabisa nawahakikishia kuwa nitaendelea kuwa sauti yenu Bungeni na kuwawakilisha ipasavyo kwa Unyenyekevu,Utiifu,Uadilifu na Uaminifu mkubwa.
*MUHIMU:* Natoa wito kwa watumishi wote na viongozi ngazi za Vijiji na Kata kuhakikisha kuwa miradi hii iliyoletewa fedha inasimamiwa vizuri na kwa ufanisi mkubwa ili wananchi wapate huduma hizi kwa wakati.
*SingidaMasharikiSSH2025*
*Mungu Ibariki Singida Mashariki*!
*Mungu Ibariki Tanzania* !
*Mungu ambariki Mhe. Rais wetu Mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.*
*Imetolewa na Ofisi ya Mbunge*
*Mh Miraji Jumanne Mtaturu* (Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki)
*Leo tarehe 9. 1. 2024*
*Kazi Iendelee*