Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea taarifa ya uandishi wa kitabu cha ‘Miaka 60 ya Ofisi ya Makamu wa Rais‘ kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (wa nne kushoto) ofisini kwake Ikulu Chamwino mkoani Dodoma Januari 05, 2024. Wengine alioambatana nao ni Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi wa kitabu hicho Bw. Rawson Yonazi (wa pili kushoto), Mshauri wa kamati Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Muungano – Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Hanifa Selengu (wa kwanza kushoto).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake Ikulu Chamwino mkoani Dodoma na kuwasilisha taarifa ya uandishi wa kitabu cha ‘Miaka 60 ya Ofisi ya Makamu wa Rais‘
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi wa kitabu cha ‘Miaka 60 ya Ofisi ya Makamu wa Rais‘ Bw. Rawson Yonazi (wa kwanza kulia) baada ya kupokea taarifa ya uandishi wa kitabu hicho ofisini kwake Ikulu Chamwino mkoani Dodoma Januari 05, 2024. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi wa kitabu cha ‘Miaka 60 ya Ofisi ya Makamu wa Rais‘ Mshauri wa kamati Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kupokea taarifa ya uandishi wa kitabu hicho ofisini kwake Ikulu mkoani Dodoma Januari 05, 2024. Wengine wa pili kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga, Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi wa Kitabu Bw. Rawson Yonazi na Kaimu Mkurugenzi wa Muungano – Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Hanifa Selengu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi wa kitabu cha ‘Miaka 60 ya Ofisi ya Makamu wa Rais‘ Bw. Rawson Yonazi, (kulia) Mshauri wa kamati Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Hanifa Selengu baada ya kamati hiyo kuwasilisha taarifa ya uandishi wa kitabu hicho ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Chamwino mkoani Dodoma Januari 05, 2024.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)