Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ikiongozwa na Mwenyekiti Deus Clement Sangu (Mb) yashiriki semina ya mafunzo kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina leo tarehe 05 Januari 2024. Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika katika ukumbi wa Benki ya Tanzania (BOT) Jijini Dar-es-salaam.
Msajili wa Hazina, Ndg.Nehemia Msechu amefungua mafunzo hayo na kutoa mada inayohusu “Tathimini ya Utendaji wa Taasisi na ufanisi wa Usimamizi wa Taasisi za Umma. Wakufunzi wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Uwekezaji Ndg. Lightness Mauki pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sheria Ndg. Serephine Tamba.