Meneja wa Elfazi Hotel Christopher Yotham akisoma risala kwenye hafla ya ibada ya kutoa sadaka kwa wajane na yatima
Mchungaji Paulo Joshua akihubili kwenye ibada ya kutoa sadaka kwa wajane na yatima iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Elfazi Hotel.
Mchungaji Paulo Joshua akikabidhi madaftari na kalamu kwa mtoto yatima
Wanafunzi wenye uhitaji kutoka shule ya msingi Mhandu iliyopo Kata ya Mahina Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza wakiwa kwenye hafla ya ibada ya kutoa sadaka kwa wajane na yatima
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Jamii imeombwa kuwa na moyo wa kuwakumbuka, kuwasaidia na kuwathamini wajane na yatima kwakuwapa mahitaji muhimu ikiwemo chakula,mavazi na vifaa vya shule ili waweze kutimiza ndoto zao.
Ombi hilo limetolewa na Mchungaji Paulo Joshua alipokuwa akihubili kwenye hafla ya ibada ya kutoa sadaka kwa wajane na yatima iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Elfazi Hotel.
Amesema unapowasaidia watu wenye uhitaji unakuwa umeweka akiba kwa Mungu hivyo watu mnapaswa mjitoe kwa kadiri mlivyojaliwa kwaajili ya kuwasaidia yatima na wajane.
“Mkurugenzi wa Elfazi Hotel amewapa thamani kubwa wajane na yatima na hii mbegu aliyoipanda itazaa matunda mazuri katika kizazi kijacho hivyo ukitaka kufanikiwa kwenye shughuli zako na maisha kwa ujumla mshike mkono mjane au yatima msaidizi hakika mambo yako yatenda vizuri kuliko kawaida” amesema Mchungaji Joshua
George Peche ni mwenyekiti wa mtaa wa Kagomu uliyopo Kata ya Mahina Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, amesema Mkurugenzi wa Elfazi Hotel amefanya jambo zuri la kuwapa tabasamu watoto yatima na wajane .
“Tangu Mkurugenzi huyu alipoanza uwekezaji katika mtaa wangu amekuwa akishirikiana na sisi katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuhakikisha tunapata maji,umeme pamoja na kutusaidia kukarabati barabara za mitaa yetu hususani katika kipindi cha mvua”, amesema Peche
Kwaupande wake Prisica John mjane alieachiwa watoto sita amemshukuru Mkurugenzi wa Elfazi kwanamna anavyowasaidia yeye na watoto wake huku akiwaomba wadau wengine kujitokeza kwajili ya kuwawezesha mitaji ili waweze kufanya biashara.
Awali akizungumza kwenye hafla ya ibada ya kutoa sadaka kwa wajane kwaniaba ya Mkurugenzi wa Elfazi Hotel Meneja wa Hotel hiyo Christopher Yotham, amesema lengo la kutoa sadaka kwa wajane na yatima ni kurudisha shukurani kwa jamii kutokana na mafanikio wanayoendelea kuyapata.
Amesema wataendelea kutoa msaada kwa wajane na yatima ikiwemo kuwalipia watakofaulu mwakani kuanzia kidato cha kwanza hadi chuo bure,kutoa mitaji kwa wajane ili iwasaidie kufanya biashara ndogo ndogo pamoja na kusaidia kujenga barabara za mitaa na miundombinu ya shule.