Na Issa Mwadangala
Hayo yamesemwa Disemba 20, 2023 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya baada ya ukaguzi wa paredi la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake na kisha kufanya baraza na Maafisa , Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali.
Kamanda Mallya amewasisitiza viongozi wanao wasimamia Askari katika kutekeleza majukumu kuhakikisha wanatenda kwa uadilifu ili kuleta matokeo chanya na kupunguza malalamiko dhidi ya Jeshi la Polisi.
Naye, Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gallas Hyera amesisitiza na kukemea mambo kadha wa kadha yakiwemo askari kuacha kujihusisha na vitendo ambavyo vinaleta taswira mbaya kwa Jeshi la Polisi na kuwataka kufanya kazi kwa kufuata wimbo wa maadili ya Afisa wa Jeshi la Polisi ambao unasisitiza nidhamu, haki, weledi na uadilifu.
Jeshi la Polisi nchini limejiwekia utaratibu wa kukutana na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali mara kwa mara katika mabaraza na vikao kazi kwa lengo la kukumbushana majukumu ya kazi na kuweka mipanga mkakati ya utendaji kazi ikiwemo kuzuia na kutanzua uhalifu.