Naibu Waziri wa kilimo ,David Silinde akizungumza katika mahafali hayo ya chuo cha uhasibu Arusha
Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha ,Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza katika mahafali hayo .
Wahitimu wa chuo cha uhasibu Arusha wakimsikiliza mgeni rasmi katika mahafali hayo.
Julieth Laizer ,Arusha .
Serikali imekipongeza chuo cha Uhasibu Arusha kwa kuja na mabadiliko ya mitaala ya elimu katika upande wa kilimo, Biashara ,ufundi,utalii ambayo kwa kiasi kikubwa inayoakisi mazingira halisi ya kuisaidia Tanzania katika ukukuzaji wa uchumi.
Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa fedha wakati akizungumza katika mahafali ya 25 ya Chuo cha Uhasibu Arusha yenye wahitimu 5387 yaliyofanyika Katika hoteli ya Ngurdoto wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Amesema serikali imewekeza fedha nyingi katika vyuo vya elimu ya kati na vyuo vikuu, kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watanzania wanapata elimu bora na yenye usawa.
“Niseme chuo kimeona mbali kwa kuanzisha mitaala yenye kukidhi huhitaji, na kuwa mstari wa mbele katika kuongeza idadi ya wanafunzi,kuanzisha mitaala na fani zinazojibu changamoto kwa Taifa hili, ninawapongeza sana kwa mpango huu ” amesema .
Silinde ametoa rai kwa Taasisi ya elimu za juu kufanya tafiti na kuanzisha mitaala itakayotoa majawabu na kujibu changamoto zinazolikabili Taifa , ili wahitimu hao waliopata elimu wakalete matokeo chanya ya utekelezaji wa malengo ya millennia”amesema Silinde .
“Nafahamu kila mmoja amefanya tafiti kama takwa la chuo kabla ya kuhitimu, ni imani yangu kila mhitimu aishirikishe jamii yake ,na kutokufungia matokeo hayo kabatini, tumieni utafiti mlioufanya ili kuongeza tija katika mabadiliko yakiuchumi.”amesema .
Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha (IAA) Profesa Eliamani Sedoyeka amesema chuo icho kwa sasa kina jumla ya kozi 71 ambapo 16 stashahada, 17 stashahada, uzamili 14,shahada 24 .
Ameeleza chuo kimeanzisha shahada mpya ya medua bainowai na mawasiliano ya umma, kutokana na mazingira ya Sasa kupitia msisisitizo wa serikali katika sekta ya elimu yakutengeneza kada ya viongozi katika eneo hilo katika usimamizi wa shule na maafisa elimu ngazi ya wilaya .
“Serikali iliwapatia chuo hiki shilingi 48 bilioni na mipango ni kukakikisha chuo kinatoa misingi ya weledi na umahiri na kuwa kinara katika maeneo yote , huku mipango mikakati ya miaka 5 ni kuongeza wigo wa kujenga miundombinu ya kufundishia,kituo cha tehama, kumbi pacha za kufundishia katika kampasi 4 ya Arusha,Babati, Dar es salaam, Dodoma na tuna mpango wa kuanzisha kampasi nyingine mpya ya Songea ambapo tayari tumepatiwa shilingi 22 bilioni na serikali kwa ajili ya kujengwa kampasi hiyo ili kutengeneza soko lenye uhakika.”amesema.
Hata hivyo ili kuhakikisha usalama wa Raia na mali zao zinalindwa wameimarisha mahusiano na chuo cha polisi Moshi kwa kuja na kozi mbalimbali kwa lengo la kuvifikia vyombo vya ulinzi na usalama.
Makamu Mwenyekiti wa baraza la uongozi wa chuo hicho CPA Joseph Mwigune amesema mahafali hayo ya 25 ni dhihirisho la jitihada na mchango mkubwa kutoka kwa menejimenti ya Chuo kwa kusimamia majukumu yao ipasavyo ,kiutendaji nakuwezesha kupata ongezeko la wanafunzi .
Ameongeza kuwa, chuo kimekuwa na mipango mikakati ya muda mrefu,na mfupi waliyojiwekea ya kutoa mafunzo,utafi na ushauri wa kitaalamu katika kuendana na Sayansi na teknolojia katika kulinda Taswira na hadhi ya Chuo icho kwa wakati wa Sasa na ujao.