Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Isack Njenga akizungumza na wageni waalikwa katika hafla ya kusherehekea Miaka 60 ya Uhuru wa Kenya iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es Salaam Desemba 13, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Kenya katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es Salaam Desemba 13, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo kulia na Balozi wa Kenya Mh. Isack Njenga wakigonganisha glasi ya mvinyo kuashiria sherehe za miaka 60 ya Uhuru wa Taifa la Kenya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo kushoto akifurahia zawadi ya picha mara baada ya kukabidhiwa na Balozi wa Kenya Mh. Isack Njenga katima sherehe za miaka 60 ya Uhuru wa Taifa la Kenya.
……………………………
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM
Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuwa na ushirikiano na serikali ya Kenya katika kuhakikisha wanatengeneza mazingira rafiki kwa wafanyabiashara kufanya kazi zao kwa uhuru bila kuwekewa vikwanzo jambo ambalo litasaidia Bara la Afrika kuwa uhuru kiuchumi.
Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho miaka 60 ya Uhuru wa Kenya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, amesema kuwa serikali ya Kenya na Tanzania ni marafiki wa asili ambao wamekuwa wakishirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara.
Profesa Kitila amesema kuwa serikali ya Kenya na Tanzania wanafanya biashara kubwa na kufikia shilling trillioni 1.8.
“Siku ya leo inakumbusha mapambano ambayo Kenya ilifanya katika kuhakikisha inajikomboa kutoka mikononi mwa wakoloni” amesema
Profesa Kitila.
Amesema kuwa nchi ya Kenya imepiga hatua kubwa katika maendeleo kutokana wametoka mbali katika kuhakikisha wanafanikiwa.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Isack Njenga, amesema kuwa katika kusherekea miaka 60 ya uhuru wamefanikiwa kupiga hatua ikiwemo kuwa uhuru katika masuala ya kiuchumi.
Balozi Mhe. Njenga amesema kuwa wemekuwa na uhuru wa kufanya mipango na mikakati ikiwemo kuwa na dira ya maendeleo katika kufikia malengo.
“Tumekuwa tukishirikiana na nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania kwani tumekuwa na urafiki wa jadi ambao umetuwezesha kufikia malengo makubwa” amesema Balozi Mhe. Njenga.
Amesema kuwa wameweza kupinga na umaskini na ujinga na kufanikiwa kuanza kujenga viwanda pamoja na kutengeneza mifumo ya teknolojia ya kurudisha pesa kwa njia ya mtandao kutoka sehemu moja kwenda nyengine.
“Tumefanya ubunifu mkubwa wa kimataifa ikiwemo kubuni M Pesa ambao unatumiwa na watu wengi katika mataifa mbalimbali, hivyo tumekuwa tukisonga mbele”amesema Balozi Mhe. Njenga.
Ameeleza kuwa Lengo ni kuona Tanzania na Kenya inaendelea kushirikiana na kutengeneza njia mbalimbali za mashirikiano ya biashara na kutengeneza ajira kwa wananchi wake.