Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Starcare ya nchini India wakifanya upasuaji mdogo wa moyo wa kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu (Aortic Valve) bila kufungua kifua (Transcatheter Aortic Valve Implantation procedure – TAVI) katika kambi maalumu ya siku mbili ya matibabu ya moyo inayofanyika JKCI. Upasuaji huo mdogo wa kubadilisha valvu umefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.
Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Starcare ya nchini India wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kumfanyia mgonjwa upasuaji mdogo wa moyo wa kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu (Aortic Valve) bila kufungua kifua (Transcatheter Aortic Valve Implantation procedure – TAVI) katika kambi maalumu ya siku mbili ya matibabu ya moyo inayofanyika JKCI. Upasuaji huo mdogo wa kubadilisha valvu umefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.
Picha na JKCI