Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga, Mary Isango, akimpatia nyaraka mbalimbali, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mtae kilichopo Lushoto mkoani Tanga, Shafii Makamba (kulia), wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba vyenye thamani ya Sh.Milioni 114 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kununulia vifaa hivyo kupitia MSD kwenye tukio la makabidhiano lililofanyika Disemba 9, 2023. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni Dereva wa MSD, Rashidi Msambo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtae, Andrew Kilama.
…………………………………………………
Na Dotto Mwaibale, Lushoto
SERIKALI imetoa Sh.Milioni 114 kwa Kituo cha Afya Mtae kilichopo Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga ambazo zimetumika kununulia vifaa tiba kupitia Bohari ya Dawa (MSD) na hivyo kinatarajia kuanza kutoa huduma ya upasuaji mwishoni mwa mwezi Disemba 2023.
Hatua ya kituo hicho kuanza kutoa
huduma hiyo inatokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya
kuibadilisha zahanati ya kijiji cha Mtae kuwa Kituo cha Afya ili wananchi
waweze kupata huduma bora na karibu.
Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Shafii Makamba akizungumza wakati akipokea
vifaa hivyo kutoka MSD alianza kwa kuishukuru Serikali inayoongozwa na
Rais Samia Suluhu Hassani kupitia MSD kwa kuwezesha kutoa vifaa hivyo vya
dharura kwa ajili ya kufanya huduma ya dharura kwa wakina mama na watoto.
“Vifaa hivi tulivyovipokea leo kutoka MSD Kanda ya Tanga vitasaidia kupunguza vifo vya wajawazito na
watoto kwa sababu kabla ya hapo walikuwa wakilazimika kutembea umbali
usiopungua kilometa 65 kwenda Hospitali ya Wilaya ya Lushoto kupata huduma za
dharura hasa za upasuaji na kuwa wataachana na adha hiyo na kupata huduma hii
hapa hapa katika kituo chetu,” alisema Makamba.
Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Tanga, Mary Isango akizungumza
wakati akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Meneja wa MSD wa kanda hiyo, Sitti
Abdulrahman, alisema wamepeleka vifaa hivyo baada ya kituo hicho cha afya
kujengwa jengo la upasuaji na kupelekewa vifaa hivyo vyenye thamani ya
Sh.Milioni 114 ambavyo vinaenda kuondoa changamoto waliyokuwa wakiipata
wananchi kwenda kupata huduma hiyo mbali.
“Huduma za upasuaji sasa zitafanyika katika kituo hiki baada ya kupata
vifaa hivi ambavyo ni muhimu sana sisi kama bohari ya dawa wito wetu kwa
watendaji wa kituo hiki ni kuvitunza ili viweze kudumu muda mrefu na kuleta
tija kwa wananchi kadri watakavyokuwa wakiendelea kuvitumia kwa kuzingatia kuwa
Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuvinunua,” alisema Isango.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mtae, Beatrice Alphonce, Disifa Mdoe na
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Andrew Kilama waliishukuru Serikali kupitia MSD kwa
kuwapelekea vifaa hivyo ambavyo vitaondoa kabisa madhira waliyokuwa wakiyapata
na wakati mwingine kusababisha vifo.
“Tulikuwa na changamoto kubwa baadhi ya wajawazito walikuwa
wakijifungulia njiani kutokana na umbali mrefu wa kwenda Hospitali ya Wilaya ya
Lushoto kupata huduma lakini sasa tutakuwa tunaipata hapahapa nyumbani kwa
kweli tuna kila sababu ya kumshukuru Rais wetu mama Samia kwa kutuona na
kutuonea huruma wanawake wenzake na kama ingewezekana tungemuomba siku moja aje
hayaone kwa macho maendeleo haya aliyotuletea,” alisema Alphonce.
Alphonce alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia, Mbunge wa jimbo hilo,
Rashid Shangazi na viongozi wa wilaya hiyo kwa jitihada kubwa wanayoifanya ya
kuwaletea maendeleo hayo ambapo aliwaombea kwa Mungu awape afya na maisha
marefu.Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga, Mary Isango na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mtae, Shafii Makamba wakizipitia nyaraka hizo kabla ya kukabidhiana vifaa hivyo.Mapitio ya nyaraka hizo yakifanyika kwa pamoja kabla ya makabidhiano. Kutoka kushoto ni Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga, Mary Isango, Dereva wa MSD, Rashidi Msambo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtae, Andrew Kilama na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mtae, Shafii Makamba,Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtae, Andrew Kilama akishukuru Serikali kwa kuwapelekea vifaa hivyo kupitia MSD,Muonekano wa Zahanati ya Kijiji cha Mtae kabla ya kubadilishwa kuwa Kituo cha AfyaMuonekano wa jengo la upasuaji lililojengwa na Serikali na kuipandisha adhi zahanati hiyo kuwa Kituo cha Afya.Vifaa tiba hivyo vikitolewa kwenye gari tayari kwa makabidhiano.Vifaa tiba vikipelekwa kwenye jengo la upasuaji.Watoto wa Kijiji hicho wakishiriki kubeba vifaa hivyo.Kazi ya ubebaji wa vifaa hivyo ikiendelea.Vifaa vikibebwa.Wananchi wa kijiji hicho wakishiriki kubeba vifaa hivyo.Mkazi wa kijiji hicho, Beatrice Alphonce akiishukuru Serikali na MSD kwa kufanikisha kupatikana kwa vifaa hivyo.Mkazi wa kijiji hicho, Disifa Mdoe akipipongeza Serikali na MSD kwa kuwapelekea vifaa hivyo.Gari la MSD likiwa safarini kupeleka vifaa hivyo.