Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe ,akikagua Gwaride wakati akifunga mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT), kundi maalum BBT Jenga kesho iliyo bora operesheni miaka 60 ya jeshi hilo katika kikosi cha Jeshi 834 Makutupora jijini Dodoma.
Vijana wakipita mbele ya Mgeni rasmi kutoa heshima kwa mwendo wa pole na haraka Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe,wakati akifunga Mafunzo ya JKT kundi maalum la Jenga kesho iliyo bora (BBT) kikosi cha 834 Makutopora leo Disemba 8,2023 jijini Dodoma ikiwa ni oparesheni maalum ya miaka 60 ya Jeshi hilo.
Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga Mafunzo ya JKT kundi maalum la Jenga kesho iliyo bora (BBT) kikosi cha 834 Makutopora leo Disemba 8,2023 jijini Dodoma ikiwa ni oparesheni maalum ya miaka 60 ya Jeshi hilo.
Na. Gideon Gregory, Dodoma.
Wahitimu wa mafunzo katika ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wametakiwa kutambua thamani zao na jinsi Serikali inavyowajali katika kuboresha hali zao za kiuchumi na taifa kwani Serikali haitamani kuona jitihada na nguvu ilizoweka kwao zinaishia njiani.
Hayo yamesemwa leo Desemba 8,2023Jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe wakati akifunga mafunzo ya JKT kundi maalum la Jenga kesho iliyo bora (BBT) kikosi cha 834 Makutopola ikiwa ni oparesheni maalum ya miaka 60 ya Jeshi hilo.
“Mafunzo mliyo yapata hayakuwa mepesi hasa hapa JKT hivyo mnatikiwa kutoa heshima kwa kuhakikisha hazna ya serikali inafanikiwa kwa manufaa yenu na kwa taifa,”amesema Waziri Bashe.
Amesema Rais Dkt. Samia yuko tayari kuendeleza juhudi za kuinua uchumi wa nchi hususani kupitia vijana na programu hiyo ya BBT ambapo pia amewasisitiza kudumisha ushirikiano baina yao na Wizara ya Kilimo.
Hata hivyo amesema kuwa Serikali imetenga sh bilion 1.8 kwa ajili ya vijana wa program ya Jenga kesho iliobora waliohitimu leo Mafunzo hayo kwa ajili ya kuanza kuendesha kilimo.
Waziri Bashe amesema fedha hizo zitasaidia kwenye mradi mzima wa BBT ili kuhakikisha vijana wanakuwa sawa ikiwemo kuanza Kilimo kwa ajili ya kurudisha kile walichopewa na serikali.
“Fedha ziko tayari kwa ajili ya mradi wa BBT hivyo nahitaji kuona vijana jitihada zenu zinasonga mbele,”amesema Waziri Bashe.
Katika hatua nyingineWaziri Bashe amewahasa wananchi kuona fursa zilizopo kwenye kilimo kwani kimekuwa uti wa mgongo pamoja na kutoa rai kwa vijana kuchangamkia fursa pale wanapozipata na kuzitumia kutimiza malengo yao.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema program hiyo imekuwa ya viwango vya juu hivyo vijana hao wanapaswa kuzingatia walichofundishwa.
Amesema kuwa wakati wanaanza Mafunzo waliitwa Kuruta lakini hivi sasa jina hilo haliwafai tena badala yake wataitwa service Man na Service Girl.
“Tumefurahi sana kupata vijana hawa wa Mafunzo tunasubiri awamu nyingine ili tuweze kuwapa Mafunzo na nidhamu kwenye Kilimo,”amesema Meja Jenerali Mabele.
Naye Kaimu Kamanda wa JKT 834 Makutupora Meja James Macheta,amesema kuwa wamefurahi sana kupata watu wa Mafunzo kwa ajili ya kujifunza masuala ya Kilimo.
Meja Macheta amesema kuwa JKT ni sehemu sahihi ya watu kufanya mabadiliko yao kwenye nyanja tofauti ikiwemo kilimo.
Nao wahitimu wa mafunzo hayo wamesema wakati wakiwa katika mafunzo hayo wamejifunza masomo mbalimbali kwa nadharia na vitendo ambayo yamewafanya kuwa wazalendo, watii, wenye nidhamu, wachapakazi, wakakmavu na wenye fikra chanya kwa taifa.