“Waandishi wa habari ni vyema kuzingatia usalama wako kwanza wakati unatekeleza majukumu yako ya kukusanya taarifa sehemu zenye vurugu au sehemu nyingine ni bora kujiangalia wewe kwanza na sio kuhatarisha maisha yako katika mazingira hatarishi ambayo yanaweza kukusababishia madhara ambayo unaweza kuyaepuka” Alisema.
Kamanda Mallya Alihitimisha kwa kuwasihi waandishi wa habari kujikita katika kujielimisha kitaaluma na kujua mipaka ya kazi yao pindi wanapotimiza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii juu ya uhalifu kwa njia ya mtandao ili jamii ipate kuelewa.
Kwa upande wa waandishi wa habari wamelishukuru Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe kwa elimu waliyoipata na wamemuomba Kamanda Mallya kuendeleza kudumisha ushirikiano uliopo kati yao na Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe