Baadhi ya Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania wakiwa katika foleni ya mchakato wa taratibu za kuvuka mpaka wa Burundi walipowasilia katika mpaka wa Tanzania na Burundi.
Na; Mwandishi Wetu – Bujumbura, BURUNDI
WAJASIRIAMALI zaidi ya 300 kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania kushiriki maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika Bujumbura, Burundi kuanzia tarehe 5 hadi 15 Desemba, 2023.
Maonesho hayo yanafanyika katika Viwanja vya Cercle Hyppique (Golf Course), Bujumbura yakiongozwa na kauli mbiu isemayo ‘Kuunganisha Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki kufanya biashara katika eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki’.
Baadhi ya Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania wakiwa katika foleni ya mchakato wa taratibu za kuvuka mpaka wa Burundi walipowasilia katika mpaka wa Tanzania na Burundi.
Baadhi ya Wajasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupata vibali vya kuvuka mpaka wa Burundi.
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)