Makamu wa Rais FIDA Laura Nyirinkindi akiongoza mjadala katika mkutano wa Wanasheria Wanawake na watetezi wa haki za binaadamu katika kuadhimisha miaka 20 ya Jumuiya ya Wanasheria Wanawake uliofanyika Golden Tulip Kiembe samaki Zanzibar.
Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Suza PROF.Mohammed Makame Haji akiongoza mjadala katika mkutano wa Wanasheria Wanawake na watetezi wa haki za binaadamu katika kuadhimisha miaka 20 ya Jumuiya ya Wanasheria Wanawake uliofanyika Golden Tulip Kiembe samaki Zanzibar.
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binaadamu Zanzibar Juma Msafiri Karibona akichangia mjadala katika mkutano wa Wanasheria Wanawake na Watetezi wa Haki za Binaadamu katika kuadhimisha miaka 20 ya Jumuiya ya Wanasheria Wanawake uliofanyika Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Mwenyekiti wa Wajane Zanzibar Tabia Makame akichangia mjadala katika mkutano wa Wanasheria Wanawake na watetezi wa haki za binaadamu ikiwa ni maadhimisho ya kutimiza miaka 20 ya Jumuiya ya Wanasheria Wanawake uliofanyika Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Mshauri wa Jinsia Ofisi ya Tume kuu ya Haki za Binaadamu EARO Catherine De Preux Baets akichangia mjadala katika mkutano wa Wanasheria Wanawake na watetezi wa haki za binaadamu ikiwa ni maadhimisho ya kutimiza miaka 20 ya Jumuiya ya Wanasheria Wanawake uliofanyika Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Yumna Mmanga akichangia mjadala katika mkutano wa Wanasheria Wanawake na watetezi wa haki za binaadamu ikiwa ni maadhimisho ya kutimiza miaka 20 ya Jumuiya ya Wanasheria Wanawake uliofanyika Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano wa Wanasheria Wanawake na watetezi wa haki za binaadamu ikiwa ni maadhimisho ya kutimiza miaka 20 ya Jumuiya ya Wanasheria Wanawake uliofanyika Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Afisa Sheria kutoka Idara ya katiba na Msaada wa Kisheria Ali Haji Hassan mjadala katika mkutano wa Wanasheria Wanawake na watetezi wa haki za binaadamu ikiwa ni maadhimisho ya kutimiza miaka 20 ya Jumuiya ya Wanasheria Wanawake uliofanyika Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Naibu Mkuu wa Skuli ya Sheria Msemo Semvua Mavare akiwasilisha mada katika mkutano wa Wanasheria Wanawake na watetezi wa haki za binaadamu ikiwa ni maadhimisho ya kutimiza miaka 20 ya Jumuiya ya Wanasheria Wanawake uliofanyika Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Na Fauzia Musaa, Maelezo
Mkurugenzi Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanziabr Jamila Mahmoud amesema Jumuiya hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza upatikananji wa haki za Wanawake na usawa wa kijinsia.
Akizungumza katika Mkutano wa Wanasheria Wanawake na Watetetezi wa haki za Binaadam uliofanyika Golden Tulip Bi jamila amesema ZAFELA itaendelea kushirikiana na Taasisi za Kiserikali na Binafsi ili kueneza uelewa kuhusu sheria za Zanzibar na kuhimiza ushiriki wa Wanawake katika kuunda sheria zinazogusa maisha yao.
Aidha alisema Jumuiya hiyo itaongeza jitihada katika kuhamasisha na kuwawezesha Wanawake na Watoto kuelewa, kutetea, na kukuza haki zao kupitia kampeni za vyombo vya habari, juhudi za utetezi, utafiti, mijadala ya umma, pamoja na mitandaoya kijamii.
“ Dira ya jumuiya hii inahusisha haki, usawa, utawala wa sheria, na msaada wa kijamii kwa wote, hususan wanawake na watoto wasiojiweza ndani ya Zanzibar” Alifahamisha Bi Jamila
Alieleza kuwa Mkutano huo wa kutimiza miaka 20 ya ZAFELA ulilenga kuwajengea uwezo na kuimarisha nafasi ya Mwanamke katika Taaluma ya sheria na utetezi wa haki za binadamu .
Aliongezea kuwa wakati Zafela inaadhimisha Miaka 20 tangu kuanzishwa kwake jumuiya hiyo imepiga hatua katika upatikanaji wa haki, kuongeza uelewa juu ya haki za wanawake, kupiga vita ukatili wa kijinsia (GBV) pamoja na kutoa huduma za usaidizi wa kisheria kwa wanawake wasiojiweza na watoto wenye uhitaji Zanzibar.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binaadamu Zanzibar Juma Msafiri Karibona amesema Tume hiyo itaendeleza mashirikiano na Taasisi nyengine za Sheria ili kuhakikisha haki za Binaadamu zinazingatiwa na kupatikana kwa Ufanisi.
amesema mashirikiano hayo yamekuwa yakisaidia katika kuhakikisha haki za Wanawake , watoto na watu wenye mahitaji maalum zinapatikana ikiwemo kushirikishwa katika kila harakati za kijamii.
Aidha ameeleza kuwa Tume hiyo imekuwa ikifanya uchunguzi wa mambo mbali mbali na kuyatolea ufumbuzi ili kuweza kuzishauri Serekali zote mbili juu ya mamabo hayo na kuhakikisha haki za Binaadamu zinapatikana.
Akizungumzia suala la Udhalilishaji alisema licha ya jitihada zinazochukuliwa za kupambana na suala hilo, bado limekuwa ni changamoto hivyo alishauri kuongeza nguvu za pamoja katika kumaliza janga hilo.
Nao baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo akiwemo Mkurugenzi wa Wajane Zanzibar Tabia Makame alisema bado wajane na watoto wanakosa haki zao ikiwemo haki ya matunzo hivyo aliwaomba watetezi wa haki za Binaadamu kuhakikisha haki hizo zinapatikana baada ya kuachana na wenza wao.
Alisema suala la kuelemewa na mzigo wa matunzo na malezi ya watoto kwa wajane kunachangia kuathirika kisaikolojia na kuongeza idadi ya Wagonjwa wa Akili katika Hospitali za Afya ya akili Zanzibar .
Hata hivyo alisema baadhi ya Wanawake wapo nyuma katika kujishirikisha na kujitolea kushika nafasi mbali mbali jambo linalopelekea kukosa haki zao na kuwataka kuacha kukaa nyuma na badala yake kuzikimbila fursa hizo .
Mkutano huo wa siku tatu ulifungulia rasmi disemba 30 mwaka huu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwashirikisha Wanasheria wa kike, watetezi wa haki za Binadamu, wanaharakati wa haki za Wanawake, Sekta binafsi, Mahakama na Watendaji akuu wa Serikali kutoka ndani na nje ya Zanzibar.