****
Wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo wilaya ya Shinyanga (Shinyanga District Council SACCOS Limited) wamekutana kujadili ajenda mbalimbali za uendeshaji wa chama hicho ulioambatana na uchaguzi wa viongozi, wajumbe na kamati ya usimamizi.
Mkutano huo wa mwaka wa chama Shinyanga District Council SACCOS Limited umefanyika leo Jumamosi Disemba 02, 2023 katika ukumbi wa mikutano ofisi za halmashauri uliopo manispaa ya Shinyanga.
Akisoma taarifa ya mwaka wa 2023 ya chama cha Shinyanga District Council SACCOS Limited aliyekuwa mwenye kiti wa chama cha kabla ya kumaliza muda wake wa uongozi Deus Muhoja ameeleza mafanikio waliyoyapata kwa kipindi cha muda husika na kubainisha changamoto zinazokwamisha uendeshaji wa vikundi vya akiba na mikopo ni pamoja na liba kubwa kwenye taasisi za kifedha (Benki) pindi wanapoitaji kuchukuwa mikopo.
“Chama cha SDC SACCOS kimeendelea kujiendesha kwa faida na kukuza mtaji kwa kuendelea kutoa huduma ya mikopo kwa wanachama, chama kimeweza kununua hisa 4,000 tokabenki ya ushirika KCBL za kiasi cha Tsh 2,000,000/=, lakini pia kimeweza kutoa mikopo kwa njia ya ukokotoaji wa punguzo la kila mwaka (REDUCING BALANCE) na kuongeza muda wa mkopo kutoka miaka 5 hadi 8, ni matarajio yetu kuendelea kushusha riba ya mikopo kwa wanachama hadi kufikia chini ya asilimia 10 ikitegemeana na hali ya biashara itakapokuwa nzuri”,amesema Deus Muhoja.
“Lakini pia tutaendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya ushirika , matumizi sahihi ya mikopo na umuhimu wa wanachama kujiwekea akiba na amana, changamoto kwenye vyama vya akiba na mikopo ni ukubwa wa riba wakati wa kuomba mikopo kwenye taasisi za kifedha (benki) imekuwa kikwazo kwa sababu wao wanakopesha kwa asilimia ya riba 14-18 lakini sisi wananchama wetu tunawakopesha kwa asilimia 12 atutaweza kutengeneza faida tutakapowakopesha wanachama wetu”,ameongeza Deus Muhoja.
Akisoma taarifa ya kamati ya usimamizi ya chama cha Shinyanga District Council SACCOS Limited kuanzia Januari 01 hadi Septemba 30, 2023 katibu wa kamati hiyo Festo Stanslaus amesema mpaka sasa chama hicho kina jumla ya wanachama 205 huku akieleza akiba na hisa za wanachama hadi kufikia Tsh. Milioni 70.25.
Aidha Chama cha akiba na mikopo wilaya ya Shinyanga (Shinyanga District Council SACCOS Limited) kimefanya uchaguzi wa viongozi wapya baada ya kufikia ukomo wa uongozi wa miaka mitatu kulingana na katiba ya chama hicho ambapo wanachama wamefanya uchaguzi wa kuchagua viongozi mbalimbali akiwemo mwenyekiti, makamu mwenyekiti, wajumbe na kamati ya usimamizi.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo mwenyekiti wa uchaguzi ambaye pia ni afisa ushirika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Shija Mwika amemtangaza Epafras Mazina kuwa mwenyekiti wa Chama cha akiba na mikopo wilaya ya Shinyanga kwa kupata kura 54, Aisha Omary kuwa makamu mwenyekiti kwa kupigiwa kura za ndio huku wajumbe wakiwa ni Betha Lazaro, Kulwa Maige na Mathias Balele.
Kwa upande wa kamati ya usimamizi mwenyekiti akichaguliwa Editha Emmanuel, katibu akiwa Festo Stanslaus na mjumbe ni Pili Magai.
Baadhi ya wanachama waliohudhuria mkutano mkuu wa 21 wa chama hicho.
Wajumbe wa Chama cha akiba na mikopo wilaya ya Shinyanga (Shinyanga District Council SACCOS Limited)waliomaliza muda.
Mwenyekiti, Makamu na Wajumbe wapya wa Chama cha akiba na mikopo wilaya ya Shinyanga (Shinyanga District Council SACCOS Limited) waliochaguliwa.
Mwenyekiti aliyechaguliwa Epafras Mazina.Makamu Mwenyekiti aliyechaguliwa Aisha Omary (KUSHOTO) akiwa na Mjumbe Betha Lazaro.
Mwenyekiti wa mkutano mkuu wa 21 wa Chama cha akiba na mikopo wilaya ya Shinyanga (Shinyanga District Council SACCOS Limited) Christian Kitojo akizungumza wakati wa mkutano huo.