Mratibu wa usugu wa Vimelea vya maradhi Wizara ya Afya Zanzibar Muhidin Omar akiwasilisha mada ya usugu wa vimelea vya maradhi dhidi yadawa kwa Waandishi wa habari wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa yaliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
Mwandishi wa habari wa ZBC Radio Hinja Pongwa akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari juu ya usugu wa vimelea vya maradhi dhidi ya dawa yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
Afisa Habari kutoka Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Mwantanga Juma akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari juu ya usugu wa vimelea vya maradhi dhidi ya dawa yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
Mwandishi wa habari wa Zanzibar Cable Malik Shaharan akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari juu ya usugu wa vimelea vya maradhi dhidi ya dawa yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la kiengereza la Daily News Issa Yussuf akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari juu ya usugu wa vimelea vya maradhi dhidi ya dawa yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Na Imani Mtumwa, Maelezo
Mratibu wa Usugu wa Vimelea vya Maradhi Wizara ya Afya Dk. Muhidini Omar ameitaka jamii kutumia Dawa kwa usahihi ili kupunguza ongozeko la Maradhi katika jamii.
Akizungumza wakati akitoa Mafunzo kwa Waaandishi wa habari juu ya Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo amesema jamii imezowea kutumia dawa bila ya kuonana na Daktari jambo ambalo linapelekea kuharibu Afya za Wananchi.
Akifafanua kuhusu dhana ya Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa alisema ni pale dawa zilizokuwa zikitumika awali kushindwa kutibu Maradhi ya kuambukiza kama vile Kifua kikuu, Nimonia na Ukimwi .
Hata hivyo alisema miongoni mwa visababishi vya usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa ni pamoja na mazingira ni ukataji miti ovyo na muingiliano wa watu hupelekea kuengezeka kwa Maradhi.
Aidha alisema kwa Zanzibar asilimia 90 ya vimelea vimeonyesha Usugu dhidi ya Dawa ambazo zinatumika kutibu maradhi mbali mbali kwa uzembe hivyo aliisisitiza jamii kutumia dawa kwa kuzingatia maelekezo ya daktari ikiwemo kukamilisha dozi ili kupunguza ongezeko la vifo katika nchi yetu.
Kwa upande wake Daktari Mkuu wa Mifugo Idara ya Mifugo Zanzibar Dr Ali Zahran amesema miongoni mwa sababu kubwa zinazochangia usugu wa vimelea dhidi ya maradhi ni pamoja na Wanyama kwani wafugaji hawataki kufuata ushauri wa daktari katika kuwatibu wanyama jambo ambalo linapelekea kwa Usugu wa Maradhi.
Alifahamisha Serikali imeweka vituo 11 vya kutibu wanyama na vituo zaidi ya 10 binafsi hivyo amewataka wafugaji na wakulima kuvitumia vituo hivyo ili kulima na kufuga kiutalamu ili kumlinda Mtumiaji.
Kwa upande wao Washiriki wa Mafunzo hayo wamesema wataifanyia kazi Elimu hiyo kwa kutoa taarifa na kufanya vipindi mbali mbali vinavyohusiana na usugu wa vimelea dhidi ya dawa kwa jamii ili ipate kuelimika juu ya tatizo hilo.
Hata hivyo wameitaka Wizara ya Afya na Wizara ya Kilimo na Mifugo kushirikiana vyema na Waandishi wa Habari ili kuhakikisha tatizo hili linaloikumba jamii linapungua kwa wananchi kwa kuwapatia elimu yakutosha ili kupunguza Maradhi na Vifo.
Mafunzo hayo ya siku moja yaliwashirikisha Waandishi wa Habari,Wataalamu wa Afya,na pamoja na wataalamu kutoka Idara ya Mifugo Zanzibar.