Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Pro.Muhammed Makame Haji akimkabidhi jezi Kepteni wa timu ya mpira wa miguu ya wafanyakazi wa SUZA Hamiar Sleiman Hamiar wakati wa hafla ya Suza Sports Day iliyofanyika Uwanja wa Skuli ya Afya Mabweni
Wafanyakazi wa SUZA na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Hicho wakicheza Mchezo wa kuvuta kamba katika siku ya Suza Sports Day iliyofanyika Uwanja wa Skuli ya Afya Mabweni Zanzibar,ambapo wafanyakazi wa suza walifanikiwa kuwavita suzaso.
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar Pro.Mohammed Makame Haji akizungumza na wachezaji wa Timu ya mpira wa miguu ya wafanyakazi na Serikali ya wanafunzi wa Suza katika hafla ya Suza Sports Day iliyofanyika Uwanja wa Skuli ya Afya Mabweni
Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Na Imani Mtumwa , Maelezo
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Prof Mohammed Makame Haji amesema kuwepo kwa michezo katika Sekta ya Elimu kutasaidia Wanafunzi kuimarisha Afya zao
Akizungumza wakati akifungua Bonaza la Michezo la SUZA Sports Day huko katika Viwanja vya Skuli ya Afya Mbweni amesema Bonaza hilo litawafanya Wanafunzi kuweza kuepukana na Maradhi yasioambukiza kama vile kisukari na presha.
Aidha alisema kutokana na kuona umuhimu wa Michezo wameamua kuweka siku maalum ya Michezo SUZA ili kuweza kudumisha michezo ndani ya chuo hicho.
Hata hivyo ameeleza kuwa katika chuo hicho wanafunzia wa kike wamekuwa na muamko wa kushiriki michezo kutokana na chuo hicho kuwapa kipaombele kwa kuwawekea michezo inayoendana nao ikiwemo mpira wakikapu na wavu.
Kwa upande wake Waziri wa Michezo wa Serekali ya Wanafunzi SUZASO Ali Shaali amesema wataendeleza michezo katika chuo hicho kwa kuwashirikisha vijana wote wakiwemo wenye ulemavu ili kuwapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao.
Aidha alisema wataendelea kushajihisha vijana kushiriki katika siku hiyo kwa kujiongezea nafasi za kujitangaza kwani Michezo ni ajira.
Nao baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika michezo hiyo walisema wataendelea kushiriki katika michezo ili kuimarisha Afya zao na kujikinga na maradhi mbalimbali yasioambukiza kwani michezo ni afya .
Katika Bonaza hilo wanafunzi wa SUZA walishiriki michezo mbali mbali ikiwemo uvutaji wa kamba.kufukuza kuku,pamoja na mpira wa miguu kati ya watendaji na seriksli ya Wanafunzi ya chuo hicho.