Na.Ashrack Miraji Same- kilimanjaro
Mbuge wa jimbo la Same Mashariki Mhe. Anne Kilango amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani kwa kitendo cha kistoria kuendelea kuthamini wananchi jimboni kwake Same Mashariki Mkoani Kilimanjaro.
Ametoa pongezi hizo wakati wa makabidhiano ya Gari la kubeba wagonjwa Katika kituo cha afya Ndungu, gari itakayo saidia kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji baada ya kukosa huduma hiyo kwa miaka mingi.
“Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassani imenifanyia mambo mengi katika jimbo langu ikiwemo kujenga vituo vya Afya, miundombinu ya Barabara na miradi ya elimu na hiki kinacho fanyika Leo kukabidhiwa Gari pia leo la wagonjwa katika kituo cha Afya Ndungu ni Jimbo pekee kwenye Mkoa wa kilimanjaro ndiyo limepewa Gari hilo kwa lengo la kuwasaidia wananchi”.Alisema Mbunge huyo wa jimbo la Same Mashariki.
“Gari hili ni kwa ajili ya kuboresha huduma ya Mama na mtoto pia litatumika kuwahudumia wagonjwa hakika imani yangu na serikali kwa ujumla ni kuokoa Maisha ya wananchi wa jimbo la Same Mashariki hivyo ni msaada mkubwa Sana katika jimbo langu na kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.
Baadhi ya wananchi wa tarafa ya Ndungu wamemuomba Mhe. Mbuge Kilango kufikisha Salamu za Shukran kwa Waziri wa Tamisemi na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzanian Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassani kwa kutatua kero kubwa Katika jimbo hilo kutokana na ukubwa wa jimbo lenyewe pia serikali kuendelea kuwatazama kwa jicho la upekee na kuongeza Gari lingine