Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohamed Mussa (kushoto)akisalimiana na Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Zhang Zhisheng mara baada ya kuwasili Ofisini kwake na Ugeni kutoka Manispaa ya Jiji la Chongqing Nchini China ukiongozwa na Naibu Meya Shang Kiu kwa ajili ya kuimarisha Udugu na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Michenzani Mall.
Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohamed Mussa akitoa hotuba ya makaribisho kwa Wageni kutoka Manispaa ya Jiji la Chongqing Nchini China wakiongozwa na Naibu Meya wa Jiji hilo Shang Kiu baada ya kuwasili Ofisini kwake kwa Ziara maalum ya kuimarisha Udugu na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Michenzani Mall.
Baadhi ya Wageni kutoka Manispaa ya Jiji la Chongqing Nchini China waliofika Ofisini kwa Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar kwa Ziara maalum ya kuimarisha Udugu na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Michenzani Mall.
Naibu Meya wa Jiji la Chongqing Nchini China Shang Kiu akizungumza baada ya kuwasili Ofisini kwa Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohamed kwa Ziara maalum ya kuimarisha Udugu na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Michenzani Mall.
Naibu Mkurugenzi Baraza la Jiji la Zanzibar Said Salum Ufuzo akitolea maelezo Mji wa Zanzibar kwa Wageni kutoka Manispaa ya Jiji la Chongqing Nchini China waliofika Zanzibar kwa Ziara maalum ya kuimarisha Udugu na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Michenzani Mall.
Wageni kutoka Manispaa ya Jiji la Chongqing Nchini China wakiwa pamoja na wenyeji wao waheshimiwa mbalimbali wa manispaa za Zanzibar wakisikiliza Hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Hussein Ali Mwinyi kupitia Luninga inayohusiana na Jiji la Zanzibar walipofika katika Ofisi Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar katika Ziara maalum ya Kuimarisha Udugu na kubadilishana Uzoefu katika utendaji kazi ,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohamed katikati akizungumza na Wageni kutoka Manispaa ya Jiji la Chongqing Nchini China baada ya kufika Ofisini kwake kwa ajili ya Ziara maalum ya kuimarisha Udugu na kubadilishana uzoefu hafla ilifanyika katika ukumbi wa Ofisi hio Vuga Jijini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohamed akimsikiliza Naibu Meya wa Jiji la Chongqing Nchini China Shang Kiu akimuonesha kitu katika Kitabu baada ya kufika Ofisini kwakwe na Ugeni aliofatana nao kwa Ziara maalum ya kuimarisha Udugu na kubadilishana uzoefu hafla ilifanyika katika ukumbi wa Ofisi hio Vuga Jijini Zanzibar.
………………..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mh. Masoud Mohamed ameahidi kudumisha ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kukuza uchumi wa Nchi.
Akizungumza na Naibu Meya wa Manispaa ya Jiji la Chong Qing kutoka China huko Ofisini kwake Vuga amesema Serikali ya Zanzibar na Serikali ya China ni marafiki wa muda mrefu hivyo wataendelea kushirikiana ili kuleta maendeleo katika nchi.
Amesema ugeni huo una lengo la kuzisaidia manispaa katika kubadilishana uzoefu wa iutendaji kazi ili kuhakikisha jiji la Zanzibar kuwa na mazingira mazuri.
“Kama tunavyoelewa kuwa wenzetu wa Jamhuri ya Watu wa China wamepiga hatua kubwa sana katika kuipendezesha miji yao” alisema
Aidha amefurahishwa na ujio huo pamoja na kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kendelea kuunga mkono Juhudi za Serikali ya Zanzibar katika kuleta maendeleo nchini.
Nae Naibu Meya wa manispaa ya jiji la Chong Qing Hon. Shang Kiu ameahidi kuwa ushirikiano huo utakuwa endelevu ili kuleta nufaaa katika nchi zote mbili.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohamed
Mussa, amesema ugeni huo una nia dhabiti ya kushirikiana na kusaidiana kwa pamoja ili kupendezesha Mji wa Zanzibar.
Aidha, amesema katika kupendezesha Mji wa Zanzibar kuwa safi kunahitajika kupata miundombinu itakayoweza kusaidia kuimarisha Nchi..
Ugeni huo ulikuwa nchini kwa siku mbili na ulitembelea maeneo mbali mbali kwa ajili ya kuangalia mazingira ya mji na utalii ulipo Zanzibar.