Na Dotto Mwaibale, Singida
KAMATI
ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa skimu ya
umwagiliaji uliopo Kijiji cha Msingi Kata ya Msingi wilayani Mkalama mkoani
Singida ambao serikali imetoa zaidi ya Sh. Bilioni 34.
Akizungumza
wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani Mkalama Mwenyekiti wa kamati Daniel
Sillo aliipongeza Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji (NIRC) chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Raymond Mndolwa kwa kazi kubwa
inayoifanya ya kukamilisha miradi hiyo ya ujenzi wa mabwawa ambayo ni muhimu
kwa Taifa ukiwemo mradi huo wa Skimu ya Umwagiliaji Kata ya Msingi Mkalama.
Sillo alisema
kukamilika kwa mradi huo kutaongeza pato la mtu mmoja mmoja na
taifa kwa ujumla na kuwa mradi huo na mingine yote itakapo kamilika
inakwenda kuchangia ongezeko la fedha katika bajeti ya Serikali.
Sillo alisema miradi hiyo inatekelezwa kwa maagizo ya Rais Samia Suluhu
Hassan ambaye anataka kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza
uzalishaji kwa wananchi kupitia kilimo cha umwagiliaji.
Aidha, Sillo aliwataka wananchi wasijenge kwenye eneo la mradi hasa kwenye
mashamba yanayotarajia kulimwa kwani mradi huu ukikamilika utawanufaisha wao
kwa kulima zaidi ya mara moja kila mwaka .
Sillo aliiomba Wizara ya Kilimo hasa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kusimamia vizuri mradi huo na
kukamilika kwa wakati ili uwe na tija kwa wananchi na Taifa.
Naye Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amempongeza Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa
ya Umwagiliaji . Raymond Mndolwa kwa kusimamia vizuri ujenzi wa miundombinu ya
umwagiliaji.
Silinde alisema serikaki inataka wananchi walime si kwa kutegemea mvua na
kwamba mradi huo utakapokamilika utaongeza pato la mwananchi sababu atakuwa
anavuna zaidi ya mara mbili kwa mwaka na pia itaongeza pato kwa halmashauri na
usalama wa chakula nchini.
Akizungumzia suala la wananchi kuanza kujenga katika mashamba, Silinde alisema ni kwasababu wanafahamu nini kinakwenda kutokea na kuwataka waache serikali
itengeneze miundombinu ya mradi huu kwani lengo la serikali ni kuondokana
kwenye kilimo cha kienyeji kuja kwenye kilimo cha kisasa chenye tija.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Raymond Mndolwa, alisema ujenzi wa mradi huo utakapokamilika unatarajia kuwanufaisha zaidi ya
wakazi 12,000 wa vijiji vinne vilivyopo Kata ya Msingi.
Aidha aliieleza kamati hiyo kuwa wananchi wameanza kujenga nyumba kwenye
eneo la mradi huo hivyo kuanza kupoteza eneo la kilimo ambapo aliomba eneo la uwekezaji
thamani yake ni vema likabaki lile lile vinginevyo manufaa ya uwekezaji itakuwa
ni bure.
suala hili kwa kuwazuia wananchi wasiendelee kujenga mashambani kwani Sh.Bilioni
34 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya mradi huu ni fedha nyingi.
kama ilivyopangwa na kuwa miradi yote inayojengwa itakamilika kwa wakati na
serikali inaendelea kutoa fedha kwa aajili ya utekelezaji.
Awali Mkurugenzi wa Idara ya Ukarabati na Ujenzi wa Miundombinu, Mhandisi Fuko Koyoya, alisems
mradi huu ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 18 utawanufaisha wakazi
12,000 wa vijiji vinne vya Ishinsi, Ndurumo, Msingi na Kidi vilivyopo Kata ya
Msingi tarafa ya Kinyangiri ambao watalima mazao ya mpunga,mahindi na mbogamboga
Kwa misimu miwili hadi mitatu kwa mwaka.
Alisema shughuli zitakazofanyika katika mradi huu ni ujenzi wa bwawa lenye
ujazo wa Lita 1,875,000, ujenzi a mifereji ya umwagiliaji yenye kilometa 19.12,
uchimbaji wa mifereji ya matupio yenye urefu wa kilo mita 42.539, uchimbaji wa
mifereji ya kuingiza Maji mashamba yenye urefu wa jumla ya kilometa 34.778.
Shughuli nyingine zitakazofanyika ni ujenzi wa barabara za mashamba zenye
urefu wa kilomita 36.1, kusawazisha ekari 2,000 za mashamba,ujenzi wa kilomita
nane za barabara na makaravati sita kuelekea ndani ya mradi na ujenzi wa vigawa
Maji 14,vipunguza mwendo,viumbo angalizi 90,vipitisha maji 90,makaravati 14
pamoja na vivuko nane.
Mradi huo ambao umeanza kujengwa Julai Mosi mwaka huu unatarajia kukamilika
Disemba 14, 2024.
Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Francis Isack, akishukuru Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huo ambao ni muhimu kwa wananchi na taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali (kulia) akizungumza wakati akiwakaribisha wajumbe wa kamati hiyo.
Safari kuelekea ulipo mradi huo ikifanyika.