Serikali kupitia Wizara ya Maji imedhamiria kumaliza kabisa changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa Maji safi na Salama katika wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro mpango unaoendana na kukamilisha mradi mkubwa wa Maji Same, Mwanga-Korogwe.
Mpango huo ni miongoni mwa maadhimio yaliyo fikiwa baada ya kikao kazi kilicho fanyika mjini Dodoma baina ya Waziri wa Maji (MB) Jumaa Aweso aliembatana na watendaji walio katika sekta hiyo akiwemo naibu katibu, wabunge wa majimbo yote mawili ya Same Mashariki na Same Magharibi, mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni na watendaji wengine wa mamlaka za maji wa wilaya ya Same na wamkoa wa Kilimanjaro.
“Nitumie fursa hii kushukuru serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo kupitia wizara ya Maji iliyo chini ya Waziri Jumaa Aweso kudhamiria kuondoa kabisa shida ya Maji kwenye wilaya ya Same mimi kama msimamizi mkuu kwenye wilaya ya Same matumaini yangu ni kuwa wananchi wataendelea na shughuli za uzalishaji kwa uhuru zaidi kwakua Maji ni kati ya hitaji muhimu zaidi kuchochea maendeleo”.Alisema mkuu wa Wilaya ya Same.
“Niendelee kuwashukuru watendaji na viongozi wenzangu kwa ushirikiano uliopo hususani katika kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali, ahadi yetu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia suluhu Hasani na serikali yake ni kuongeza ufanisi kwenye usimamizi wa fedha zinazo letwa kwenye wilaya ya Same kuhakikisha zinatumika kwa kwa malengo yaliyokusudiwa kuboresha huduma na kuharakisha maendeleo ya wilaya yetu.