WAJUMBE WA KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakikagua utekelezaji wa Ujenzi wa miradi ya Umwagiliaji Shamba la Mbegu Ngaramtoni Arusha pamoja na shamba la Mbogamboga Tengeru.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Daniel Siro na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mkoani Manyara ameshika mche wa zao la mchikichi
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti akiwa amefurahi jambo huku akiwa ameshilia mche wa mchikichi ulipo katika shamba la wakala wa mbegu Ngaramtoni Arusha.
WAJUMBE WA KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt Sophia Kashenge juu ya mtambo wa kuchakata mbegu .
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Daniel Siro akipata maelezo juu ya ghala la kuhifadhi mbegu mbalimbali kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt Sophia Kashenge
Na Lucas Raphael,Arusha
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeridhishwa na usimamizi wa fedha katika utekelezaji wa Ujenzi wa miradi ya Umwagiliaji Shamba la Mbegu Ngaramtoni Arusha pamoja na shamba la Mbogamboga Tengeru yote yakimisimamiwa na Wakala wa Mbegu za kilimo ( ASA)
Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Kamati hiyo Daniel Siro na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mkoani Manyara alisema wajumbe wa Kamati hiyo wameridhishwa na miradi inayotekelezwa na Wakala wa Mbegu.
Alisema miradi hiyo ilitengewa fedha na Serikali na kamati hiyo ndio iliyosimamia utengaji wa fedha hizo hivyo kuna kila sababu ya kamati kukagua nakuona thamani ya fedha ilivyotumika katika sekta ya Umwagiliaji.
Alisema miradi hiyo Kwa Shamba la Arusha yenye thamani ya Billion 4.4 ikikamilika itaongeza upatikanaji wa Mbegu bora za kilimo Kwa wananchi na kupunguza uaigizaji wa Mbegu kutoka Nchi za nje.
Mwenyekiti huyo alisema katika sekta ya kilimo Kamati hiyo inamatumaini makubwa ya kupata matokeo chanya baada ya ukamilishaji wa miradi hiyo.
Alisema mpaka sasa Kamati hiyo baada ya kutembelea miradi ya Wakala wa Mbegu za kilimo haina mashaka ya matumizi ya fedha za umma kutokana na kuonekana kwa thamani ya fedha zilivyotumika.
Aidha aliipongeza Kampuni inayojenga miundombinu hiyo ya Umwagiliaji Pro Agro Global ltd kwa kufanya kazi Kwa uzalendo na kuonesha kuwa vijana wakipewa kazi wanaweza.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt Sophia Kashenge alisema Wakala wanaishukuru Kamati ya bajeti kwa kutembelea miradi hiyo na kutoa ushauri pamoja na kuona thamani ya matumizi ya fedha za umma.
Alisema lengo la Miradi hiyo nikuongeza Uzalishaji wa Mbegu Nchini ili kupunguza uaigizaji wa Mbegu kutoka Nchi za nje.
Dkt, Sophia alilishukuru Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla Kwa kuona umuhimu wa kuongeza bajeti ya wizara ya Kilimo na vile vile kuona umuhimu wa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya Umwagiliaji hasa katika mashamba ya mbegu.
Alisema ili Wakala wa Mbegu uweze kufikia malengo yake inabidi Mashamba yake yote yawekewe miundombinu ya Umwagiliaji ili kuwe na Uzalishaji wa Mbegu wa uhakika kwa msimu wote wa mwaka mzima .
“Kufika kwa Kamati hiyo ya Bajeti ni faraja kwetu lengo letu waone matamanio ya Taasisi inapotaka kufika kwenye uhakika wa Miundombinu ya Umwagiliaji ilituweze kujitosheleza katika uzalishaji wa mbegu” alisema Dkt, Sophia.