Mkurugenzi Mkuu wa Mahakama ya Biashara na Kituo cha Kimatifa ya Usuluhishi (IAC) iliyopo nchini Kazakhstan Almat Igenbayev (kushoto) akionyesha ujumbe wa Mahakama ya Tanzania mmoja ya Maktaba ya kuhifadhia kumbukumbu mbali wakati walipotembea Kituo hicho jana kwa ajili ya kupata uzoefukuhusu usuluhishi.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mahakama ya biashara na Kituo cha Kimatifa ya Usuluhishi (IAC) iliyopo nchini Kazakhstan Almat Igenbayev (katikati) na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho cha Mahakama ya Tanzania Mh.Dkt. Angelo Rumisha(kulia) mara baada ya kutembelea Mahakama hiyo jana kwa ajili ya kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya usuluhishi.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mahakama ya Biashara na Kituo cha Kimatifa ya Usuluhishi (IAC) iliyopo nchini Kazakhstan Almat Igenbayev (kulia) mara baada ya kutembelea Mahakama hiyo jana kwa ajili ya kubadilishana uzoefu kuhusu usuluhishi.
Mwanasheria kutoka Mahakama ya Kimatifa ya Biashara na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi (IAC) iliyopo nchini Kazakhstan (mwenye koti la Kaki) Aidana Rassova akitoa maelezo kwa ujumbe wa Mahakama ya Tanzania uliongozwa na Mtendaji Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel walikuwa na ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu jana katika Mahakama hiyo kuhusu usuluhishi katika kutatua migogoro katika masuala ya biashara na uwekezaji.
NA Tiganya Vincent- ASTANA- Kazakhstan
Ujumbe wa Mahakama ya Tanzania ukiongozwa na Mtendaji Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel umetembelea Mahakama ya Kituo cha Kimataifa cha Biashara Astana na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi kilichopo nchini Kazakhstan kwa lengo ya kubadilishana uzoefu kuhusu njia za usuluhishi katika utatuzi wa migogoro ikiwemo ya kibiashara na uwekezaji katika sekta mbalimbali.
Alisema uzoefu waliopata utasaidia kuweka mipango ambayo itakiwezesha Kituo cha Usuluhishi kutumika zaidi katika utatuzi wa migogoro mbalimbali ikiwemo ile ya kibiashara, ya sekta za ujenzi na uwekezaji kwa ajili ya kuimarisha uchumi kwa kupunguza mlolongo mrefu wa kesi unaotumia njia nyingine za Mahakama.
Ujumbe wa Mahakama ya Tanzania umemaliza ziara ya mafunzo nchini Kazakhstan baada ya kutembelea Mahakama ya Upeo(Supreme Court) na kujifunza matumizi ya mifumo ya Teknolojia ya Habari katika usimamizi wa shughuli mbalimbali, kisha kukutana na Naibu Waziri wa Sheria, Bazala la Juu linalosimamia Maadili ya Majaji na kutembelea Taasisi ya Mafunzo kwa Majaji.