KLABU ya Mamelodi Sundowns imekuwa timu ya kwanza kuchukua ubingwa wa michuano ya African Football League (AFL) 2023 kwa kuichapa mabao 2-0 Wydad Casablanca.
Mamelodi wamekuwa washindi wa Michuano hiyo kwa jumla ya mabao 3-2 katika Fainali ya kwanza iliyochezwa nchini Morocco wenyeji walishinda mabao 2-1.
Kwa ushindi huo Mamelodi wamechukua kiasi cha sh.bilioni 9.9 ambapo michuano hiyo ilizinduliwa Oktoba 20,jijini Dar es Salaam kwa mechi ya Simba vs Al Ahly uliomalizika kwa timu zote kufungana mabao 2-2.
Timu zilizoshiriki ni Simba SC Tanzania,TP Mazembe DR Congo,Al Ahly Misri,Wydad Casablanca Morocco,Enyimba Nigeria,Esperance Tunisia,Petroleos De Luanda Angola na Mamelodi Sundows Afrika Kusini.