Na. Damian Kunambi, Njombe.
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa Vyandarua 26, 333 vyenye thamani ya zaidi ya sh mil. 204 kwa shule za msingi 117 zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya ludewa mkoani Njombe ili kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji vyadarua hivyo iliyofanyika katika shule ya msingi Ludewa mjini wilayani humo Meneja wa Bohari ya Dawa( MSD ) Kanda ya Iringa Robert Lugembe amesema seeikali imedhamiria ifikapo mwaka 20230 ugonjwa huo wa malaria uwe umetokomezwa kabisa.
“Serikali yetu inayoongozwa na mama yetu Samia Suluu Hassan ikasema watu wote wapate vyandarua, hapa tunafanya kwa watoto wa shule lakini kuna ugawaji mwingine unaendelea sehemu nyingine ambapo mwananchi anapata chandarua, kwahiyo kila mtu anapewa chandarua na serikali ili kuhakikisha kwamba ugonjwa wa malaria unatokomea kabisa inapofika mwaka 2030”. Amesema lugembe
Aidha kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Ahobokile Songela ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo amesema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha jamii kwa kusema kuwa vyadarua hivyo vimewekewa madawa ili vidhuru watu kitu ambacho si cha kweli.
” Ndugu zangu achaneni na imani hii potofu, hakuna kiongozi anayeweza kuwadhuru wananchi wake, hivi mnafikiri kiongozi akiwaharibu ama kuua wananchi wake yeye atakuwa kiongozi anayewaongoza akina nani? Lengo la Rais wetu Dkt. Samia Suluu Hassan ni jema na anathamini afya za watu anaowaongoza”,Amesema Songela.
Ameongeza kuwa Lengo la serikali ni kuhakikisha kwamba zero malaria inapatakina na watu wake wote wanakuwa na afya njema kwani kuwa na afya njema ni kuwa na kizazi ambacho kina nguvu na kinaweza kupeleka uchumi wa nchi katika malengo ambayo yamekusudiwa.
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Mratibu wa malaria wilayani Ludewa Erasto John amesema bado Kuna changamoto kwa baadhi ya jamii ambao wamekuwa wakibadili matumizi ya vyandarua hivyo kwa kuvulia samaki, kufugia kuku pamoja na kuzungushia bustani ambapo kaimu Mkurugenzi aliahidi kutoa elimu kwa jamii.
Nao baadhi ya wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Ludewa mjini ambako uzinduzi huo umefanyika kiwilaya wameishukuru serikali kwa kuwapatia vyandarua hivyo kuwa vinaenda kuwasaidia katika kutokomeza malaria huku uzinduzi huo ukienda sambamba na kauli mbiu isemayo zero malaria inaanza na mimi.