Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
WAFANYABISHARA
wilayani Mkuranga na Kibiti, wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa
kutuliza dhorobu ya hali ya biashara nchini.
Wamesema kwenye wilaya hizo biashara zinafanyika kwa amani na utulivu bila usumbufu tofauti na miaka ya nyuma.
Wametoa
pongezi hizo kwa nyakati tofauti kwenye mkutano kati ya wafanyabishara
wa wilaya hizo na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara (JWT)
inayoendelea mkoani Pwani yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za
wafanyabishara.
Mfanyabiashara Hassan Mbwana Kambangwa, amesema
wafanyabiashara kwa asilimia kubwa wilayani humo wananufaidika sana
tangu kuingia kwa utawala wa Rais Samia.
Amesema “Kimsingi
namshuruku Rais Samia kwa kutuletea ugeni uliotupa fursa ya kuzungumza
changamoto zinazotukabili, lakini sisi tangu kuingia kwa utawala huu wa
Mama Samia tunafaidika nao kwa asilimia kubwa.”
Mfanyabiasha huyo
ametolea mfano wa mambo wanayofaidika nayo kuwa ni mikopo, uhusiano
mazuri na halmashauri lakini pia taasisi mbalimbali za kifedha ziko huru
kuwasaidia wafanyabiashara.
Amesema serikali imezingatia suala
la amani na utulivu na kwa mikoa mingi ilikua inapata changamoto nyingi
lakini hapa wilaya ya Mkuranga wafanyabiashara wako huru na
wanafanyabiashara bila bugudha.
“Tunamshukuru sana Rais Samia
Suluhu Hassan tunafanyabiashara kwa amani lakini pia tunashukuru ujio
huu wa leo umefanya tuweza kufunguka yale ambayo yako ndani ya moyo na
tunaamini mtayafikisha,” Kambangwa.
Naye mfanyabishara Wilaya ya
Kibiti, Salim Juma, amempongeza Rais Samia kwa kuona sekta ya
wafanyabishara ni sehemu ya uchumi wa Taifa na kuamua kuungana kwa
pamoja kutatua kero zao.
“Ili kuwa na ustawi tumefanikiwa kumpa
Rais Samia, ambaye ameona umuhimu wetu na kutambua mchango wetu ndio
maana leo viongozi mpo hapa,” amesema Juma.