Mkuu wa mkoa wa Arusha ,John Mongela akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha.
Rais wa taasisi hiyo akizungumza katika kongamano hilo mkoani Arusha .
Julieth Laizer,Arusha .
Arusha .Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amefungua kongamano la sita la Taasisi ya Wataalamu wa udhibiti wa rushwa na ufisadi Tanzania (ACFE-T) mkoani Arusha .
Aidha Mongela ameipongeza serikali na mifumo yake kukubali uwepo wa Taasisi hiyo ambayo imeanza kuingia kwenye mifumo ya serikali Kwa kufanya kazi kizalendo.
Amesema ameona mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Hussein Ally Hassan Mwinyi Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar wakifanya mambo kubwa sana wakipeleka fedha nyingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kutokana na wanadamu kuwa na mapungufu na kutokamilika kiutendaji ni vema kama nchi ikawa na mifumo imara inayokubalika kimataifa ili kuendelea kukidhi matakwa na viwango vya kimataifa zaidi.
Amesema kuwa ni vema viongozi na wahasibu ,vyombo vya uchunguzi,jeshi la polisi Takukuru,wakapewa mafunzo maeneo ya kazi kutokana na unyeti wa kada hizo.
Kwa upande wake Ali Mabrouk Juma Rais wa Taasisi ya ACFE Tanzania Chapter amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na vita ya vitendo vya rushwa.
Amesema kuwa ,kongamano hilo limehusisha wataalamu mbalimbali vikiwemo vyombo vya Dola ili kuwajengea uwezo katika kupambana na vitendo vya rushwa maeneo ya kazi.
Hata hivyo kongamano hilo limekuja na mada mbalimbali ikiwemo ya kukemewa vitendo vya rushwa na ufisadi,vitendo vya utakatishaji fedha na zinginezo .
Amesema kuwa bado taasisi hiyo haijatambulika kitaaluma Katika muundo wa watumishi serikalini na Kukosa chombo maalumu cha kuwasimamia jambo ambalo amesema ni muhimu kama nchi Sasa kuitambua taasisi hiyo.
Mmoja wa wawezeshaji katika kongamano hilo, CFE Pauline Mtunda ambaye ni Kiongozi mkuu wa taasisi ya Hillcrest Auditors amesema kuwa katika mafunzo hayo wanataka kuangalia ni namna gani na kujadili namna ya kusaidia serikali katika maswala ya uchunguzi kwenye maeneo ya kimaendeleo.
Amesema kuwa atazungumzia majukumu ya bodi katika kupingana na maswala ya ufisadi ,sasa bodi ndio wanasimamia maswala ya gorvanance kuangalia mashirika na taasisi zinavyopaswa kuendeshwa.
Amesema kuwa wanapaswa wawe na uelewa wa namna juu namna gani weka miundombinu ya kusimamia na wana majukumu ya kuhakikisha uelewa na mafunzo katika taasisi unakuwepo ili kuweza kubaini mianya ya ubadhirifu kabla haujatokea.
Sisi kama chama tunaamini kuwa kukiwepo na miundombinu mizuri haya maswala ya ubadhirifu yanaweza kugundulika mapema kabla hayajatokea swala sio kusubiri tatizo litokee ndio tufanye uchunguzi bali tunapaswa kuwa na miundombinu ya kugundua kabla tatizo halijatokea.
Ameongeza kuwa, ukiangalia kwenye shughuli za miradi ya maendeleo asilimia karibia 70 ya fedha za umma zinapelekwa kwenye miradi ya maendeleo huko ndiko kuna manunuzi na kwenye manunuzi huko ndiko kuna changamoto hata ukiangalia zile ripoti za CAG zinaonyesha fedha zilizotengwa kwenye miradi fulani mradi umefanyika lakini fedha haziendani hivyo watafundisha namna bodi itakavyosimama katika maeneo hayo.