Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ametoa wito kwa waumini wa Msikiti wa Sanya Juu Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuliongoza taifa kwa amani na utulivu.
Dkt. Mollel ametoa wito huo katika maadhimisho ya Siku ya Elimu ya Dini katika Msikiti wa Sanya Juu wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro.
Dkt. Mollel amesema Taifa lenye amani na utulivu wananchi wake wanafanya kazi kujipatia kipato ili kuleta maendeleo ya taifa lao.
“Rais Samia ni kiongozi imara na shupavu hivyo watanzania ni kumtia moyo kwa kumuombea ili awezetimiza yale alopanga kuyatekeleza katika kuleta maendeleo kwa watanzania na Tanzania isonge mbele”, ameeleza Dkt. Mollel.
Aidha Dkt. Mollel ameupongeza uongozi wa Msikiti huo kwa kuwalea watoto katika maadili mema na kusema kuwa hao ndo viongozi wa kesho watakao kuja kulitumikia taifa.
Vile vile amewatia moyo walimu wanao fundisha watoto katika msikiti huo kwa kuwapatia kiasi cha shilingi million moja ili kuendelea kuwafundisha watoto hao kwani ndio taifa la kesho.