Na Ahmed Mahmoud
Bunge la Afrika Mashariki EALA limejadili maboresho ya kanuni Miongozo na sheria za uendeshaji wake utakaosaidia kuongeza ufanisi wa shughuli zake.
Akiongea mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa kwanza wa kikao cha pili cha bunge la Tano la EALA Jijini Arusha Mbunge wa Bunge hilo kutoka Kenya kennedy Kalonzo Musyoka amesema kwamba yapo yaliojadiliwa ambayo mengine hawajakubaliana.
Kwa Mujibu wa Musyoka amesema yale ambayo hawajakubaliana ikiwemo kuwepo kwa Naibu spika itapelekea kupiga kura ili kuweza kuyapitia au kutopitisha hivyo suala hilo litangojea uwepo huo.
“Tumekuwa katika kikao cha leo tukijadili marekebisho ya kanuni Miongozo na sheria za uendeshaji wa Bunge la EALA yapo tuliokubaliana na mengine hatujakubaliana mfano suala la kuwa na msaidizi wa spika hilo halijapita hadi tutakapopiga kura”
Hata hivyo kwa muda mrefu tumekuwa na changamoto ya Mawaziri kutohudhuria vikao eidha hawaji wanashughuli nyingi za serikali zetu hili linasababisha shughuli za Bunge hili zinazorota hivyo tunaomba wajitahidi kuja tusaidiane katika hii Kazi ya Jumuiya.
Kwa Upande wake Mbunge wa Bunge hilo kutoka Kenya David Ole Sankok amezitaka nchi za EAC kujenga ushirikiano katika Mtangamono wa forodha ya Pamoja kwa kutembeleana bila kuwa na mipaka sababu hii mipaka iliwekwa na wakoloni.
Alisema suala la mtangamono wa Sarafu ya pamoja lakini viwango vya fedha zetu hazivilingani katika nchi zetu saba Kuna fedha ipo na nguvu na nyingine ipo chini kidogo lazima tuweze kuzilinganisha ndio tuwe na EAC shilingi ifikapo mwaka 2031 lakini kabla ya kufika huko tunatarajia tuanze kwa kutumia fedha zetu za ndani kwa biashara zetu za nchi za Jumuiya.
“Kwa sababu hakuna haja ya Mruwanda kubadilisha faranga kwa Dola ya Kimarekani ndio afanye biashara Tanzania kwani akifika Tanzania itambidi abadilishe Dola kwa fedha ya Tanzania hii ni kupoteza fedha nyingi sawa na asilimia 10 tunapoteza fedha nyingi baada ya Makato kwa biashara tulionayo baina ya nchi zetu sawa na bilioni 71 za kimarekani ukitoa asilimia 10 ya fedha hiyo ni ni nyingi kuliko bajeti zetu”
Vilevile tuwe na soko ambalo ukiuza bidhaa za mipakani hakuna haja ya kubadilisha fedha zetu kwa Dola ya Kimarekani kwani watu wetu wengi wale wanaofanya biashara wengi ni wajasiriamali wadogo wakulima wafugaji na wengine hawajasoma ukiwaambia wabadilishe pesa kwa fedha za nje kabla hawajavuka mpaka itakuwa ni vigumu kufanyabiashara tunataka kuwawezesha kufanya biashara.