Mkurugenzi Mkuu Benki ya Dunia anayeshughulikia masuala ya Afya Dkt. Juan Pablo akizungumza kuhusiana na ziara yao ndani Zanzibar,ambapo alisema lengo la ziara hiyo ni kuangalia hatua iliyofikiwa katika uboreshwaji wa huduma za Afya ya mama na mtoto .
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na ujumbe kutoka Benki ya Dunia unaoshugulikia masuala ya Afya kuhusiana na mambo mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za Afya Zanzibar.
Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Zanzibar Sleiman Salim (kushoto)akifanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu benki ya Dunia anayeshughulikia masuala ya Afya Dkt. Juan Pablo kuhusiana na ziara yao ndani ya Zanzibar,ambapo alisema lengo la ziara hiyo ni kuangalia hatua iliyofikiwa katika uboreshwaji wahuduma za Afya ya mama na mtoto .
Meneja Mkuu anaeshughulikia masuala ya Afya, Lishe na idadi ya watu Kusini na Mashariki mwa Afrika Dr.Emest Massiah(kulia) akizungumza kuhusiana na ziara yao ndani ya Zanzibar,ambapo alisema lengo la ziara hiyo ni kuangalia hatua iliyofikiwa katika uboreshwaji wa huduma za Afya ya mama na mtoto .
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt.Salim Slim akizungumza kuhusiana na ujio wa ujumbe wa Benki ya Dunia unaoshugulikia masuala ya Afya ambapo alisema lengo la ugeni huo ni kuangalia hatua iliyofikiwa katika uboreshwaji wa huduma za Afya ya mama na mtoto .
PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR
Na Imani Mtumwa, Maelezo
Wizara ya afya Zanzibar imepokea ugeni kutoka Benki ya Dunia wenye lengo la kuboresha Huduma za Afya Nchini.
Akizungumza mara baada ya kupokea ugeni huo Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Salim Slim amesema pamoja na mambo mengine ujumbe huo una lengo la kuangalia uboreshwaji wa huduma za Afya ya mama na motto.
Aidha alisema Ujumbe utafanya Ziara katika vituo vya Afya kwa ajili ya kuangalia upatikanaji wa huduma hizo pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zitakazobainika wakati wa ziara hiyo.
Alisema Wizara imefurahishwa na ujio wa ujumbe huo na kusema itaendelea kutoa mashirikiano kwa wadau hao na kufanya kazi kwa pamoja ili kuendelea kuboresha huduma za Afya Zanzibar.
Nao wajumbe kutoka Benki ya Dunia wanaoshughulikia masuala ya Afya Mkurugenzi Mkuu Dkt. Juan Pablo na Meneja Mkuu anaeshughulikia masuala ya Afya, Lishe na idadi ya watu Kusini na Mashariki mwa Afrika Dr.Emest Massiah waliitakaWizara ya Afya kuweka mikakati inayokubalika ili kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa jamii.
Awali walimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kutoa kipaombele katika Sekta ya Afya na kupambana na maradhi mbalimbali Nchini .
Hata hivyo waliishukuru Wizara hiyo kwa mashirikano yao wanayoendelea kuyaonesha kwa kila hatua za Ujumbe huo.
Wadau hao wa Afya kutoka Benki ya Dunia watafanya ziara katika vituo mbalimbali vya Afya kwa lengo la kuangalia changamoto na kuzifanyia kazi.