Katibu Tawala wa mkoa wa Tabora Dkt John Mboya akiwa wanajadiliana jambo na mratibu wa msafara wa Samia Love Lazaro Nyalandu njeofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora
Mratibu wa msafara wa Samia Love Lazaro Nyalandu akipatiwa maelezo na Daktari bingwa wa mifupa na ajali wa hospital ya Malolo, Emanuel Mtui akimpitisha sehemu mbalimbali za hospital ya malolo wanavyofanya kazi
Daktari bingwa wa mifupa na ajali wa hospital ya Malolo, Emanuel Mtui juu ya shughuli mbalimbali za kitabibu zinazofanyika ndani ya hosptali hiyo .
Na Lucas Raphael,Tabora
Serikali ya mkoa wa Tabora imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya afya kwa kuboresha huduma za afya kwenye hosptali ,Vituo vya afya na Zahanati .
Kauli hiyo ilitolewa na katibu Tawala wa mkoa wa Tabora Dkt Jon Mboya alipokuwa akizungumza na timu ya Samia Love iliyowasilia mkoani tabora kwa ajili ya kueneza ujumbe wa upendo kwa mama Kwenye Hosptali Mbalimbali Mkoani Humo.
Alisema kwamba serikali haiwezi kutekeleza kila kitu katika sekta ya afya bila kushirikiana na wadau wa maendeleo kwa ajili ya kuboresha huduma za afya .
Alisema kwamba serikali imejitaidi kuboresha mazingira mazuri kwa upande wa majengo ila vifaa tiba wadau nao wanatakiwa kuisaidia serikali kuwezesha kupata vitendea kazi vya afya.
“kuwapenda wagonjwa ni jambo jemba ambalo wauguzi na madaktari wanatakiwa kuonyesha upendo kwa wagonjwa na watendaji kuwa tayari kwa ajili ya kutoa huduma bora za kitabibu kwenye hospital zetu”.alisema Dkt Mboya
Awali Mratibu wa timu ya Samia Love, Lazaro Nyalandu alisema lengo la ziara hiyo ni kutembelea hosptali ya Malolo kuangali jinsi ngani wanaweza kuisaia kupata vifaa kwa ajili ya wagonjwa wa mifupa hasa nyonga na magoti.
Alisema kwamba kwa sasa kuna wimbi kubwa la matatizo ya nyonga na magoti na kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Tabora wanapata huduma za madaktari bingwa kwa ajili ya kutibu maradhi mbalimbali .
Alisema kwamba lengo ni kuleta tabasamu katika maisha ya watu kutokana na upendo huo wa mama licha ya gharama kuwa ni kubwa lakini upendo wa mama unaweza kuponguza gharama hizo.
Alisema kwamba kutokana na ushirikiana ulionyeshwa kati ya serikari kwa kushirikina na watu binafsi katika utoaji wa huduma za afya uingwe na uendeleae kote nchini .
Naye Daktari bingwa wa mifupa na ajali wa hospital ya Malolo Emanuel Mtui alisema kwamba hospitali hiyo imekuwa ishirikiana vizuri na serikali kwa ajili yan kutoa waganga bingwa wa magonjwa mbali mbali kwa ajili ya kusaidia wananchi wa mkoani wa Tabora.
Alisema kwamba hosptali hiyo kwa siku upokea wagonjwa wa mifupa kuanzi 20 hadi 25 na wengi wakiwa na umri wa miaka 20 hadi 35 .
Alisema kwamba hosptali hiyo itaendelea kutoa huduma za ubingwa kila mara kutokana na kutiwa nguvu na upendo wa mama ulionyeshwa na timu ya Samia Love.
Timu ya Samia Love inavijana 24 wa kujitolewa kwa ajili ya kusambaza ujumbe wa upendo kwa wagonjwa walioko kwenye hospitali mbalimbali nchini