Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye,akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia ambayo inawataka wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri nchini, kuandaa mikutano na vyombo vya habari hafla iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye,akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia ambayo inawataka wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri nchini, kuandaa mikutano na vyombo vya habari hafla iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye,wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia ambayo inawataka wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri nchini, kuandaa mikutano na vyombo vya habari hafla iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw.Mobhare Matinyi,akielezea lengo la Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia ambayo inawataka wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri nchini, kuandaa mikutano na vyombo vya habari hafla iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia ambayo inawataka wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri nchini, kuandaa mikutano na vyombo vya habari iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, John Kayombo,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dkt. Semistatus Mashimba,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Dkt. Omary Nkullo,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bi. Siwema Hamoud Jumaa,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi Zaina Mlawa ,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Shabani Millao,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Paul Sweya,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi Ally,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye,amewapongeza Idara ya Habari-MAELEZO kwa kuja na ubunifu wa kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia ambayo wakuu wa mikoa pamoja na wakurugenzi wa halmashauri nchini wataitumia kuandaa mikutano na vyombo vya habari.
Waziri Nape amezindua kampeni hiyo leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma amesema pamoja na kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita wananchi bado hawana taarifa za kutosha.
Amesema kampeni hiyo inawataka wakuu wa mikoa yote 26 na wakurugenzi wa halmashauri zote 184 nchini, kuandaa mikutano na vyombo vya habari ili kutangaza kwa wananchi kazi zinazofanywa na serikali yao.
“Programu hii ya Tumekusikia Tumekifikia, itakwenda nchi nzima ambayo lengo lake ni kufahamisha umma kazi kubwa iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na serikali ya awamu sita kwenye sekta za maji, afya, miuondombinu na miradi mingine ya maendeleo nchini”amesema Waziri Nape
Aidha amesema lengo jingine la kampeni hiyo ni kuongeza chachu ya mawasiliano katia ya wananchi na serikali yao kwa kuwa itatoa nafasi ya wakuu wa mikoa pamoja na wakurungezi kueleza mambo ambayo yamefanywa.
“Serikali inatoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mbalimbali hivyo wananchi wanayo haja ya kufahamu kodi zao zinafanya nini tunapozungumzia, maji, afya lazima waannchi wafahamu nini kinaendelea”amesema
Hata hivyo Waziri Nape amesema kupitia program wananchi watapata fursa ya kueleza kile ambacho serikali yao imefanya na kimewanufaisha kwa namna gani.
Waziri Nape ametoa wito kwa wakuu wa mikoa, wakurugenzi wa halmashauri kutoa ushirikiano kwa Idara ya Habari (Maelezo) ili kupata maudhui mazuri yatakayotumika katika vyombo vya habari.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw.Mobhare Matinyi,amesema lengo la kuanzishwa kwa kampeni hiyo ni kuwafikisha wananchi ngazi ya chini tarifa kuhusu kazi inayofanywa na serikali yao.
“Hivyo kampeni hii itasaidia kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi kuhusu kile kinachofanywa na serikali yao na kuondoa ‘gap’ lililopo hivi sasa baina ya serikali na wananchi wake”amesema Matinyi
Aidha ameeleza kuwa baada ya kuzinduliwa leo jijini Dodoma itakwenda katika mikoa yote na halmashauri zake zote 184 nchini ambapo awamu ya kwanza itakuwa ni mikoa ya Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Saalam.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kuwa Serikali imetoka zaidi ya Shilingi bilioni 81 Kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya sekta ya Elimu katika mkoa wa Dodoma ambapo imejenga Madarasa mapya zaidi ya 1400 na Shule mpya kabisa 124 na kupelekea ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na kidato Cha kwanza na Tano kuongezeka.
“Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Dkt.Samia imeufanyia mambo makubwa mkoa wa Dodoma kuanzia sekta ya afya,Elimu, barabara na maeneo mengine hivyo ndani ya miaka hii mitatu mkoa wa Dodoma unaendelea Kwa Kasi katika sekta zote tnamshukuru sana,” amesema Senyamule