Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Maonesho ya Ufugaji wenye Tija na Utunzaji wa Mazingira sanjari na kuzindua Chama cha Mazingira na Ufugaji Tija Tanzania (CHAMAUTA) katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Maonesho ya Ufugaji wenye Tija na Utunzaji wa Mazingira sanjari na kuzindua Chama cha Mazingira na Ufugaji Tija Tanzania (CHAMAUTA) katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mazingira na Ufugaji Tija Tanzania (CHAMAUTA) alipowasili kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma kwa ajili ya kuzindua
Wiki ya Maonesho ya Ufugaji wenye Tija na Utunzaji wa Mazingira sanjari na kuzindua chama hicho. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Remedius Mwema aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akitembelea na mabanda mbalimbali wakati wa Wiki ya Maonesho ya Ufugaji wenye Tija na Utunzaji wa Mazingira kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mifugo wakati wa Wiki ya Maonesho ya Ufugaji wenye Tija na Utunzaji wa Mazingira kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Maonesho ya Ufugaji wenye Tija na Utunzaji wa Mazingira sanjari na kuzindua Chama cha Mazingira na Ufugaji Tija Tanzania (CHAMAUTA) katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma Oktoba 31, 2023.
Amesema kuwa wafugaji nchini hawana budi kuwa mabalozi wazuri na kuungano mkono juhudi za Serikali za kuhifadhi mazingira kwa kufanya shughuli za ufugaji wenye tija kwa maendeleo endelevu.
Aidha, Waziri Dkt. Jafo amesema kuwa ufugaji endelevu usioathiri hifadhi ya mazingira utasaidia katika kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji nchini.
“Tuepuke migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambayo tunashuhudia ikitokea katika baadhi ya mikoa nchini husababisha kutoelewana kwa makundi haya mawili hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani, na tuna wajibu wa kulinda amani,” amesisitiza.
Kwa upande mwingine Dkt. Jafo amewahimiza wafugaji ambao wamepata ufadhili kutumia fursa ya Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mabdiliko ya Tabianchi (COP 28) kushiriki kikamilifu.
Amesema kuwa mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Novemba 28 hadi Desemba 5, 2023 utakuwa ni adhimu ya kuitangaza nchi yetu namna Tanzania inavyofanya ufugaji rafiki wa mazingira.
Hali kadhalika Waziri Jafo ametoa wito kwa CHAMAUTA kulitumia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupata uelewa kuhusu kanuni na zinazosimamia mazingira ili kuepuka shughuli zinazoharibu mazingira.
Amewataka wafugaji nchini kuunga mkono juhudi za Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anaendelea kuiletea nchi maendeleo ikiwemo kuendeleza sekta ya maji.
Amesema kupitia miradi mbalimbali Serikali imekuwa ikichimba malambo kwa ajili ya kunyweshea mifugo hususan katika maeneo yenye ukame hatua inayosaidia
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kusimamia utekelezaji wa uhifadhi wa vyanzo vya maji.
Amesema kuwa mikakati ya kuhifadhi vyanzo vya maji katika eneo la Makutupora inaendelea na kuwa tayari chanzo hicho kimeanza kutoa asilimia 61 ya mahitaji ya maji kwa mkoa.
Aidha, Mhe. Mwema amesema kuwa Serikali ya Mkoa inaendelea na Kampeni ya Kukijanisha Dodoma ambapo inaendelea kuandaa vitalu vya miche ili kukabiliana na upungufu wa miche.
Nae Mwenyekiti wa CHAMAUTA amesema chama hicho kimemtunuku Waziri Jafo kadi ya uanachama wake na mlezi kumuomba kuwa mlezi wake kutokana mchango wake na Ofisi kwa ujumla.