Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikao cha 16 cha Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya NEMC leo Novemba 1, 2023 jijini Dodoma
……………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameipongeza Bodi ya Wakurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa utekelezaji wa majukumu yake.
Ametoa pongezi wakati akizungumza kwenye kikao cha 16 cha Bodi hiyo pamoja na Menejimenti ya NEMC kilichofanyika leo Novemba 1, 2023 jijini Dodoma.
Dkt. Jafo amesifu utaratibu wa kutembelea maeneo mbalimbali kukagua shughuli za kulinda mazingira hususan katika migodi iliyopo ya mkoani Geita na kwengineko.
Aidha, ametoa rai kwa Bodi hiyo kuendelea kuisimamia NEMC inapotekeleza Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 katika maeneo mbalimbali na kuwachukulia hatua wanaoikiuka.
Amesema kuwa ni jukumu la NEMC kuhakikisha wenye viwanda, migodi na maeneo ya starehe yanafuata sheria ili kudhibiti changamoto za uchafuzi wa mazingira zikiwemo utiririshaji wa majitaka, moshi au kelele na mitetemo.
Hali kadhalika Dkt. Jafo ametoa rai kwa wananchi kufuata sheria na kuepuka vitendo vya uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji miti holela na kuacha kuharibu vyanzo vya maji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikao cha 16 cha Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya NEMC leo Novemba 1, 2023 jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Prof. Esnati Chagu akitoa neno la shukrani wakati wa kikao cha 16 cha Bodi ya Wakurugenzi wa Baraza hilo na Menejimenti ya Baraza kilichofanyika leo Novemba 1, 2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakati wa kikao cha pamoja na Menejimenti ya Baraza hilo kilichofanyika leo Novemba 1, 2023 jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)