Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati akiwasili katika Kijiji cha Masisiwe kilichopo Makete mkoani Njombe kwaajili ya kuzindua mradi wa kufua nishati ya umeme wa KV 360 unaomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Kati – Makete Dkt. Wilson Sanga wakati akikagua chanzo cha maji cha mradi wa kufua nishati ya umeme wa KV 360 unaomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) uliopo Kijiji cha Masisiwe wilayani Makete mkoani Njombe. (tarehe 27 Oktoba 2023).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kufua nishati ya umeme wa KV 360 unaomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) uliopo Kijiji cha Masisiwe wilayani Makete mkoani Njombe. (tarehe 27 Oktoba 2023).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akivuta kitambaa wakati wa kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa mradi wa kufua nishati ya umeme wa KV 360 unaomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) uliopo Kijiji cha Masisiwe wilayani Makete mkoani Njombe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wananchi wa Tandala mara baada ya kuzindua mradi wa kufua nishati ya umeme wa KV 360 unaomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) uliopo Kijiji cha Masisiwe wilayani Makete mkoani Njombe.