Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.
…………………………..
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja amewataka wanamitandao ya kijamii kuwahamiasisha wananchi ili wawajibike kulipa kodi stahiki kusaidia kusukuma mbele maendeleo ya nchi.
Hayo ameyasema leo Oktoba 23, 2023 mjini Morogoro wakati akizungumza kwenye kongamano la wanamitandao ya kijamii kuhusu Mpango Mkuu wa sekta ya maendeleo ya Fedha nchini Tanzania na sheria mpya za PPP ambapo kongamano hilo litafanyika kwa muda wa siku mbili.
“Hizo hela ambazo ni kodi zinafanya kazi nyingi ikiwemo kununua madawa hospitalini kurekebisha barabara na miundombinu mingine katika nchi unapoacha kutoa na kudai risiti tunaikosesha serikali mapato yake ambayo ni tegemeo kubwa kwa maendeleo ya nchi”amesema Mwaipaja.
Sambamba na hayo amesema serikali inakopa pesa kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya kimakati ili kuikamilisha kwa wakati ambapo mikopo hiyo inakua na makubaliano maalumu na riba ndogo.
Amesema mikopo ambayo serikali inakopa ni ile ya muda mrefu ambayo inakua na riba kidogo na inalipika kwa miaka mingi.
“Tukikopa hizi pesa ambazo unakuta riba yake ni ndogo tukajenga reli na kurekebisha bandari zetu inakua tayari tumeinua uchumi wa nchi yetu hivyo mikopo inakua na faida kubwa kwenye uchumi wa nchi”ameongeza Mwaipaja.
Amesema ili miradi ya maendeleo ifanyike na kukamilika kwa wakati ni lazima serikali ikope kwani kodi za ndani haziwezi kutosha fanya maendeleo peke yake.
Wananchi wanapaswa kutambua kuwa mikopo ni njia moja wapo ya maendeleo na mikopo mingi tunayoichukua kwa wadau wa maendeleo mingine inakua na muda wa msamaha kabla ya kuanza kurejesha (Grace Period) ya mpaka muda wa miaka 30, hivyo inasaidia kuongeza ufanisi kwenye shughuli za kimaendeleo na kijamii, ” Amesema Benny Mwaipaja.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja,akisisitiza jambo wakati akifungua Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.
Mwenyekiti wa kongamano la Wanamitandao ya kijamii Ndg Mathias Canal,akizungumza wakati wa Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.
Hope Sylus Meneja Maudhui ya Mtandaoni kutoka Global Tv na katibu wa kongamano hilo akizungumza na washiriki wa kongamano mjini Morogoro.
Katibu wa Kongamano hilo Bi.Hope Sylus,akizungumza wakati wa Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja(hayupo pichani) ,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Wanamitandao ya Kijamii na Wizara ya Fedha linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia Oktoba 23 hadi 24 , 2023.