Mafunzo kwa Watendaji na Wawakilishi wa Chama cha Kuweka na Kukopa URA SACCOS kutoka Mikoa,Vikosi na Wilaya zote Tanzania bara na Zanzibar yanaendelea Mkoani Morogoro ambapo leo Oktoba 17, 2023 ikiwa ni siku ya pili mada mbalimbali zimeendelea kuwasilishwa.
Mada zilizowasilishwa leo zililenga kuwajengea uwezo Watendaji hao ili kufanya kazi kwa weledi na kuboresha huduma zinazotolewa na Ushirika huo ambao umeendelea kuwa kinara kwa kufanya vizuri ukilinganisha na SACCOS nyingine nchini.
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Msemaji wa Jershi la Polisi Tanzania, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) David Misime ambapo aliwataka Wawakilishi hao kusikiliza maada zote kwa makini na ikibidi waulize maswali ili kupata uwelewa wa pamoja utakaopenda kuwasaidia kwenye kutoa elimu kwa wananchama waliopo kwenye maeneo yao.