Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itafanya mapitio ya Sera na mitaala ya elimu katika ngazi zote ikiwa ni jitihada ya kuwawezesha vijana nchini.
Aidha, Rais Samia amesema lengo ni kuleta mageuzi makubwa ili elimu inayotolewa kwa viajana iakisi mazingira na mahitaji ya nchi ya mandeleo na kuwawezesha wahitimu kujiajiri na kuajirika kiurahisi.
Rais Samia amesema hayo leo wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Vijana kitaifa katika Uwanja wa Kwaraa.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kuwa zaidi ya asilimia 95 ya mabadiliko ya tabianchi yanatokana na shughuli za binadamu ambazo zinaathiri misimu ya mvua na kupotea kwa vyanzo vya maji.
Rais Samia pia amesema serikali inaendelea kuchukua hatua za kuhakikisha bei ya gesi inashuka ili kuwahamasisha wananchi wengi zaidi kuacha matumizi ya mkaa ambao unaharibu ikolojia na una madhara kiafya.
Vile vile, Rais Samia amewataka wananchi hususan wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na pwani ya Bahari ya Hindi wa maeneo ya mabondeni kuchukua tahadhari dhidi ya uwezekano wa kuwepo kwa mvua za El Nino wakati wa msimu wa vuli.
Kupitia mbio za Mwenge mwaka huu, jumla ya miradi 1,424 yenye thamani ya shilingi trilioni 5.3 ilishughulikiwa katika Halmashauri 195 nchini na kati ya hiyo miradi 7 yenye thamani ya shilina dosari.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mbio za Mwenge Kitaifa 2023 kutoka kwa Kiongozi wa Mbio hizo Abdallah Shaibu Kaimu wakati wa Maadhimisho hayo katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.


[10/14, 8:03 PM] Sharifa Ikulu: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa vyeti kwa wakimbiza Mwenge Kitaifa katika Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.



