NJOMBE
Watu Sita wamefariki dunia na wengine Kumi na Mmoja kujeruhiwa katika ajali ya gari ya abiria Toyota Haisi lenye namba za usajili T733 BBP baada ya kupinduka katika kijiji cha Ndulamo wilaya ya Makete, mkoani Njombe .
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe John Imory amesema gari hilo lilikuwa limebeba abiria Kumi na Nane na kudai kwamba chanzo cha ajali ni mwendo kasi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Juma Mfanga amefika katika hospitali ambako majeruhi wamefikishwa kwa ajili ya matibabu na kisha Dkt Andrew Mombo ambaye ni kaimu mganga mkuu hospitali ya Ikonda kuthibitisha kupokea manusura na vifo vilivyotokea katika ajali hiyo
Ajali hiyo ambayo kwa kiasi kukubwa imeathiri wanachama wa chama mapinduzi waliyokuwa kwenye gari hiyo imemgusa Halima Mamuya mjumbe wa halmashauri kuu CCM Taifa aliyekuwa Makete kwa ziara ya siku moja ya kikazi ambapo anasema amehuzunishwa sana na tukio hilo ambalo limekatisha maisha ya watu kwasababu walikuwa pamoja kwenye mkutano kabla ya kukutwa na swahimu hilo