Mkurugenzi mkazi wa benki ya dunia Tanzania,Malawi,Zambia na Zimbabwe ,Nathan Balete akizungumza alipotembelea chuo cha ufundi Arusha .
Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha ,Dk Mussa Chacha akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo
Julieth Laizer,Arusha .
Chuo cha Ufundi Arusha kwa kushirikiana na Benki ya dunia wamezindua mikakati ya kuwawezesha vijana kuondokana na umaskini na kujikwamua kiuchumi na kujenga uchumi imara katika nchi za Afrika .
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mkuu wa chuo cha Ufundi Arusha ,Dk Mussa Chacha wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya vijana duniani.
Dk Chacha amesema ,endapo vijana wataelimishwa namna ya kuweza kutumia ujuzi walioupata vyuoni kutasaidia sana kuweza kuanzisha ajira zao na kuweza kuajiri wengine kwa manufaa yao na nchi kwa ujumla.
“Kwa mwaka huu benki ya dunia imeamua kuwakutanisha vijana kutoka nchi za nne lengo likiwa ni kuweza kuwaelimisha na kutoa maarifa kwao namna ya kuweza kutumia ujuzi wao kuweza kujiajiri na kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa kutengeneza ajira za kutosha.”amesema Dk Chacha.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia Tanzania ,Malawi,Zambia,na Zimbambwe Nathan Balete amesema kuwa wamefikia hatua ya kuwakutanisha vijana kutoka nchi hizo nne kwa malengo ya kuhamasisha matumizi ya ujuzi walioupata katika kushughulikia changamoto za kijamii.
Balete amesema kuwa, Benki ya dunia imetoa kiasi cha shs dola 1.5 bilioni kusaidia sekta ya elimu Tanzania ikiwa ni sehemu ya jitihada zao katika kuboresha elimu na kuwapa fursa vijana za kujifunza maswala mbalimbali yanayowahusu.
“Tutakuwa tukiendelea kufuatilia kwa karibu jinsi juhudi hizi zinavyoleta mabadiliko chanja kwa vijana na uchuminwa nchi za Afrika kwa ujumla na kuweza kutatua changamoto ya ajira ambayo imekuwa ni changamoto kubwa katika.jamii inayotuzunguka.”amesema Balete .
Nao baadhi ya vijana wakizungumzia kuhusiana na siku hiyo, Ananilea Lema na Donald Mwanatoga wamesema kuwa, mafunzo waliyopata yatawasaidia sana kuweza kujiajiri na kujikwamua kiuchumi na hata kuweza kutengeneza fursa kwa vijana wengine ambao wataweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na changamoto mbalimbali.
Lema amesema kuwa,wameweza ujio wa benki ya dunia chuoni hapo na kuweza kuzungumza na vijana hao kumeweza kuleta manufaa makubwa kwao kwa kuweza kujadili masuala mbalimbali na namna ya kuweza kujikwamua kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zilizopo nchini.