Afisa Uhusiano Mamlaka ya Reli ya Tanzania-Zambia Tazara Regina Tarimo akifafanua jambo na mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani .
Mkuu Wa Chuo Cha Teknolojia Ya Reli Mkoanii Tabora Damas Mwajanga akiwamwalisha mkurungezi mkuu wa TRC
Na Lucas Raphael,Tabora
Wakati nchi ya Tanzania ikiwa imeungana na mataifa mengine ya Afrika katika kuadhimisha wiki ya usalama wa reli ,wananchi wametajwa kuwa hatarini kuendelea kupoteza maisha kutokana na ubishi wa kufanya shughuli za kibinadamu kwa kufanya biashara na kuweka vijiwe vya kupiga soga na kupumzika katika njia za reli.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania-Zambia Tazara, Regina Albert Tarimo alipokuwa akifanya mahojiano na Waandishi wa habari katika viwanja vya chuo cha Tektenolojia ya Reli Mkoani Tabora
Alisema kwamba wananchi Kufanya biashara na mapumziko katika mazingira ya njia za reli ni makusudi ya kutekeleza ufunjivu wa kisheria kwani kuna uwezekano mkubwa wa wananchi kugongwa na treni pengine hata kusababisha ajali kufuatia uharibifu wa miundo mbinu unaotokana na shughuli zingine za kibinadamu.
“Kujenga karibu na njia ya reli ni hatari kubwa ,kuna wananchi wamekuwa wakifanya shuguli zao za kibinadamu hairuhusiwi kuchunga mifugo pia hata kulima katika maeneo ya reli”
Alisema kwamba kutokana na hali hiyo wanaendelea kutoa elimu kupitia kampeni za usalama ambazo zitawasaidia wananchi kuweza kuepukana na ajali zinazokana na uzembe .
Alisema kwamba elimu kupitia kampeni za usalama zitawasaidia wananchi kwa sababu swala la ajali limekuwa tatizo kutokana na kukatisha hovyo kwenye maugio ya reli na barabara.
“ Changamoto kubwa ni swala la Usalama ,hivyo wamekuja Mkoani hapa kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi na watumiaji wa vyombo vya moto kwa namna ya kuwa salama kwenye maeneo ya reli.
Mwakilishi wa mkurugenzi mkuu TRC na mkuu wa chuo cha chuo chaTektenolojia ya Reli Mkoani Tabora Damas Mwajanga alisema kwamba Shughuli za kibinadamu zifanyike nje na maeneo ya reli na kwa maeneo ya mjini iwe umbali angalau wa mita 20 kutoka ukingo wa reli na nje .
Alisema kwamba kwa yale maeneo ya halmashauri umbali isipungue mita 30 na kuwataka wananchi kuwa na jukumu la kulinda miundo mbinu ya reli ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea mara ajali inapotokea.
“Ili kuhakikisha usafiri wa reli unakuwa salama na wenye tija serikali ilitunga sheria ya reli namba 10 ya mwaka 2017 ,sheria hiii imejikita katika usalama na ulinzi wa miundombinu ya reli na imeweka bayana kuwachukulia hatua kali watakaofanya hujuma ya miundo mbinu ya reli”
Awali Afungua ya wiki ya usalama wa reli kitaifa yanayofanyika mkoani hapa Mkuu wa wilaya ya uyui Zacharia Mwansasu kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tabora balozi Dkt.Batilda Burian alitilia mkazo swala zima la kumekuwepo na tatizo kubwa la kutumika vibaya kwa njia za reli ikiwemo kugeuzwa kama sehemu za kupumzika ,vijiwe vya kupiga stori,njia za kupita kufanyia biashara pamoja na shughuli zingine za kibinadamu kama kilimo sanjali na kuchungia wanyama.
Madhimisho ya wiki ya usalama wa reli kitaifa yanaendelea mkoani Tabora ambayo yanafanyika kwa muda wa siku tano yakijumuisha mamlaka mbalimbali za usafirishaji.