NJOMBE
Katika jitihada za kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto pamoja adha ya kusafiri umbali mrefu kwa zaidi ya km 8 hadi 10 kufata elimu ya msingi na awal toka eneo la block X lililopo mtaa wa Kambalage hadi shule ya msingi Sabasaba na Mkombozi ziliyopo Idundilanga ,Wakazi wa eneo hilo kwa kushirikiana na serikali wameamua kubuni mradi wa shule shikizi yenye madarasa matatu ili kupunguza umbali kwa watoto wadogo
Madarasa hayo matatu yatakuwa ni darasa la awali,Darasa la kwanza,Pili na tatu ambapo serikali kupitia idara ya elimu halmashauri ya mji wa Njombe imeanzisha mradi huo ili kuwanusuru na ukatili pamoja na kusafiri umbali mrefu watoto wadogo kutoka madarasa hayo ya mwanzo katika elimu ya msingi
Baada ya kupendekeza eneo la mradi lililopo Block X ndipo Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete pamoja na wataalamu kutoka idara ya ardhi na elimu wakalazimika kutembelea na kisha kukagua eneo hilo ili kuweka mikakati thabiti ya kuanza ujenzi huo haraka iwezekanavyo.
Punde baada ya kukagua Mpete akaweka bayana mpango wa mbeleni wa kujenga ghorofa katika shule za halmahauri hiyo kwa mijini ili kutunza ardhi na kisha kueleza namna wananchi walivyopkea mradi huo kwa kuanza kuchangishana vifaa vya ujenzi na nguvu
Ofisa elimu msingi halmashauri ya mji wa Njombe Mwalimu Shida Kiaramaba amesema kutokana na uwepo wa ukatili kwa watoto mkoani Njombe ipo haja ya kujenga shule hiyo ili kuwanusuru watoto wanaotembea umbali mrefu huku afisa ardhi wa halmashauri hiyo Amosy Luhamba akisema kutokana na udogo wa eneo hilo wanaweza kuanza kufikiria kujenga shule ya Ghorofa katika siku za usoni.
Hata hivyo Diwani wa kata ya Njombe Mjini Alatanga Nyagawa na Ofisa mtendaji kata ya Njombe Mjini Enosy Lupimo wamesema walichokuwa wanapigania kwanza ni kupata eneo huku wakiwaomba wadau mbalimbali wa elimu kuwashika mkono katika kufanikisha ujenzi wa shule hiyo.
Kwa upande wao wananchi na wazazi wa eneo la Block X akiwemo Yeremia Haule na Solanus Mhagama wamekiri kuwa watoto wao wanapata adha kubwa ya kupata elimu jambo linaloweza kudidimiza ndoto zao.