WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako,akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa Mkoani Manyara
Na; Mwandishi wetu – MANYARA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwathamini vijana na kuwapa mitaji ya kuanzisha na kuendeleza shughuli za uzalishaji mali.
Prof. Ndalichako amebainisha hayo Oktoba 10, 2023 katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa Mkoani Manyara ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama aliye mwakilisha Waziri Mkuu wa Mhe. Kassim Majaliwa.
Aidha, Prof. Ndalichako amesema Mhe. Rais ameanzisha mradi wa kilimo kwa vijana wa jenga kesho iliyo bora, kuanzisha mafuzo ya unenepeshaji mifugo na ufugaji wa samaki katika vizimba ili kupata ujuzi utakaowawezesha kujikwamua kiuchumi.
Vilevile, Waziri Ndalichako amesema Mhe. Rais ametoa Shilingi Bilioni 9 kwa ajili ya kukuza ujuzi kwa vijana ambapo mwishoni mwa mwezi huu vijana 4500 wataanza mafunzo hayo.