NA STEPHANO MANGO, MBINGA
MBUNGE wa Vijana ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga KAPINGA amekuwa Mgeni Rasmi wa Maafali ya 41 ya kidato Cha nne, shule ya MKINGA SEKONDARI iliyopo Halmashauri ya Mbinga Mji Mkoani Ruvuma,
Akiwa shuleni hapo Naibu Waziri huyo wa Nishati alipata wasaa wa kupanda mti Kama alama ya uhamasishaji Jamii juu ya utunzaji wa Mazingira pamoja na kutembelea Majengo mawili yaani Hosteli ya wasichana na Madarasa mapya ya kidato Cha tano na sita.,
Naibu Waziri huyo wa Nishati akitoa hotuba yake aliwasihi wahitimu hao wa kidato Cha nne ambao jumla yao Ni 54, kuwa msingi wa Maisha yao ndio kwanza umeanza hivyo wanapaswa kusoma kwa bidii ili kuyafikia Malengo yao na kuachana Tamaa za starehe kabla ya Muda wao,
Pia kumkumbuka Mungu kwa Kila hatua zote za changamoto au Mafanikio watakazokuwa wanazipitia, Lakini kwa kutambua umuhimu wa kundi la wanawake Naibu Waziri Judith Kapinga amechangia kiasi Cha shilingi Millioni tano (5,000,000) Kwaajili ya ujenzi wa hostel mpya ya wasichana shuleni hapo,
Wakitoa salama za chama na serikali Pendo Ndumbaro ambaye ni katibu tawala wilaya ya Mbinga pamoja na Hajira Kalinga Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi-CCM wilaya hiyo wote kwa pamoja wamempongeza na wamemshukuru Sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. SAMIA SULUHU HASSAN kupitia Naibu Waziri huyo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kusimamia vyema utekelezaji wa ILANI ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 Kwaajili ya kuwaletea Maendeleo wananchi wote wa kitanzania wakiwemo wale wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Pia Kapinga amekabidhi Kompyuta na Fotokopi/Printer kwa Ofisi ya Chama Mbinga na Jumuiya Zake
Kapinga amekabidhi kompyuta nne na fotokopi/printa kwaajili ya kuimarisha utendaji kazi na shughuli za chama na jumuiya zake katika wilaya ya Mbinga.
Aidha Kapinga amekabidhi bati na vifaa vya kujenga ofisi ya kata ya CCM Litumbandyosi na amekabidhi Jezi na Mipira kwa timu sita za Litumbandyosi
Mbunge wa Vijana Taifa, Judith Kapinga, ametembelea ofisi ya Kata ya Litumbandyosi na amekabidhi bati ishirini kwaajili ya kusaidia kuezeka ofisi ya Chama katika Kata hiyo.
Pamoja na bati hizo ameahidi pia atakabidhi tena bati zingine 20, mifuko 15 ya siment, mchanga na kokoti ili zisaidie ukarabati wa Ofisi hiyo ya Chama.
Katika hatua ingine, Kapinga ameshiriki na kuwa mgeni rasmi katika fainali ya ligi iliyoandaliwa na Prisca Diwani wa Litumbandyosi.
Katika fainali hiyo,amekabidhi jezi seti sita na mipira sita kwa timu zote sita zilizoshiriki na amekabidhi shilingi 300,000 kwaajili ya kuongezea zawadi kwa timu zote sita.