Mkurugenzi wa takwimu za uchumi Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw.Daniel Masolwa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Oktoba 9,2023 jijini Dodoma kuhusu ongezeko la watalii waliongia nchini katika pindi cha kuanzia Januari hadi Agosti, 2023.
Na.Alex Sonna-DODOMA
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema idadi ya Watalii kutoka nje ya nchi kwa kipindi cha Mwezi Januari hadi Agosti Mwaka 2023 imeongezeka na kufikia 1,131,286 ikilinganishwa na watalii 900,182 walioingia nchini kipindi kama hicho hicho mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 25.7
Hayo yamesemwa leo Oktoba 9,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Takwimu za uchumi Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw.Daniel Masolwa,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ongezeko la watalii waliongia nchini katika pindi hicho.
Bw Masolwa ametaja sababu za ongezeko hilo ni uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour nchini Marekani iliyongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na nyingine ni Tanzania kuwa na vivutio vingi ikilinganishwa na mataifa mengine duniani.
Amebainisha kuwaa kuna ongezeko la watalii 231,104 sawa na asilimia 25.7 ambapo kati ya watalii wote waliongia nchini katika kipindi hicho watalii 236,047 waliingia kupitia Zanzibar ambao ni asilimia 31.1 ya watalii wote.
“Ofisi ya Taifa ta Takwimu inajukumu la kusambaza takwimu za kijamii na kiuchumi kwa mujibu wa sheria ta Takwimu sura 351 miongoni mwa taarifa hizo ni takwimu za mara kwa mara za mwenendo wa watalii waliongia nchini”amesema Bw. Masolwa
Hata hivyo amesema kuwa watalii waliongia nchini katika kipindi cha mwezi Agosti 2023, waliongezeka hadi 186,030 ikilinganishwa na watalii 158,049 waliongia nchini mwezi Agosti 2022 sawa na ongezeko la asilimia 17.7.
“Watalii 336,203 kati ya watalii wote waliongia nchini mwezi Agosti 2023 waliongia kupitia Zanzibar sawa na asilimia 29.7 ya idadi ya watalii wote”amesema Bw. Masolwa
Pia ameongeza kuwa idadi ya watalii waliongia nchini kutoa nchi zilizo nje ya bara la Afrika kwa idadi kubwa katika kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka huu ni Marekani ikiwa na jumla ya watalii 84,541.
“Mtakumbuka Filamu ya Royal Tour ilizinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani hii inaonyesha kuwa juhudi zile za Rais Samia Suluhu Hassan zimelipa kutokana na ongezeko hili”amesema
Bw.amesema kuwa mataifa mengine yaliyoleta watalii wengi nchini nyuma ya Marekani ni Ufaransa (72,009),Ujerumani (57,798),Uingereza (51,056) na Italia (51,056).
“Aidha, katika mwezi Agosti 2023 peke idadi ya watalii waliongia nchini walitoka Italia (14,986),Marekani (14,416),Ufaransa (11,997), Uingereza (9,852) na Ujerumani (9,161)”amesema
Aidha ameeleza kuwa katika kipindi cha Januari hadi Agosti Tanzania ilipokea watalii kutoka Bara la Afrika ambapo wengi wao walitoka katika nchi ya Kenya (128,753), Burundi (69,505), Zambia (38,394), Rwanda (37,269) na Uganda (4,052).
Hata hivyo, amesema sekta ya utalii ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya fedha za kigeni nchini, hivyo taasisi na kamapni zinazotoa huduma kwa watalii zinatakiwa kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa lengo la kuwavutiwa wapya na waliokuja waje kwa mara nyingine.