Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Pili Mande
………………………………….
Na Said
Hauni, Lindi.
MKULIMA wa Kijiji na Kata ya Namapwia,wilaya ya
Nachingwea mkoani Lindi, Musa Michenje (60) amefariki dunia baada ya kukatwa
mapanga na mtoto wa kaka yake aitwae Nkono Malenga (35) kutokana na ugomvi wa
kugombania mti wa mkorosho.
Taarifa kutoka kijijini humo ambazo zime
thibitishwa na uongozi wa Kata na Jeshi
la Polisi, inaeleza mauwaji hayo yamefanyika
Oktoba 4, 2023 saa 11;00 alasiri.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baadhi
ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Diwani wa Kata hiyo Omari Lingumbende
wameeleza Michenje na Malenga ni mtu na mwanawe,walikuwa wakigombea mkorosho
uliokuwa kwenye mpaka wa shamba kati ya marehemu na kaka yake Malenga.
Mashuhuda hao Yusufu Ismaili, David Michael
walisema kutokana na mkorosho huo kuwa mpakani kaka mtu Malenga aliamua
kumuachia mdogo wake Michenje.
Walisema siku hiyo Michenga akiwa anaokota
korosho kwenye mkorosho huo,mtoto wa kaka yake aitwse Nkono alifika na kumtaka
aache kuokota.
Walisema kutokana na mabishano yaliyokuwa
yamejitokeza mtoto huyo aliyekuwa na panga mkononi alianza kumshambulia baba
yake huyo mdogo kwa kumkata maeneo mbalimbali ya mwili wake na kusababisha kifo
hapo hapo.
Diwani wa Kata ya Namapwia, Omari Liungimbende
amekiri kutokea kwa mauwaji hayo na kueleza tayari mtuhumiwa amekamatwa na kukabidhiwa
Jeshi la Polisi kuendelea na taratibu zingine za kishetia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Pili Mande
amekiri kushikiliwa kwa mtuhumiwa huyo na kueleza atafikishwa mahakamani baada
ya kukamilishwa upelelezi.