Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masala amechangia mifuko ishirini ya saruji kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya Serikali ya kata ya Nyasaka wilayani Ilemela
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika mtaa wa Nyamhuge kata ya Nyasaka Mhe Hasan Masala amewapongeza wananchi wa kata ya Nyasaka kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo
‘.. Mheshimiwa diwani tumalizie jengo letu Ili viongozi na watendaji wapate sehemu nzuri ya kufanyia kazi ..’ Alisema
Mhe Masala mbali na kuishukuru Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hasan Kwa kutoa fedha za utekelezaji wa shughuli za maendeleo pia amekemea watendaji wasiotekeleza wajibu wao pamoja na kuwataka kuhakikisha wanatatua kero za wananchi
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Mhe AbdulRahman Simba ameishukuru Serikali Kwa namna inavyotekeleza miradi ya maendeleo ndani ya kata yake huku akiwataka wananchi wake kuendelea kuchangia maendeleo
Bashite Peter ni kaimu mtendaji wa kata ya Nyasaka ambapo amesema kuwa kata yake inaendelea na utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa ofisi za Serikali za mitaa minne ya Nyanda, Nyasaka, Nyasaka senta na Nyamhuge
Bi Subira Jonas ni mkazi wa mtaa wa Nyamhuge yeye amelalamikia Upatikanaji wa huduma ya Maji ya uhakika na umeme ambapo wataalam wa sekta husika kupitia ziara ya Mkuu huyo wa wilaya walizitolea utatuzi kero zote zilizowasilishwa na wananchi