Mwenyetikiti wa kamati ya ya kudumu ya bunge ya Viwanda Biashara Kilimo na Mifugo Mariam Ditopile akipongeza juhudi juu ya teknolojia ya umwagiliaji itakavyomkomboa mkulima
Naibu Waziri wa Kilimo Davidi Silinde akisitiza jambo jana wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati ya ya kudumu ya bunge ya Viwanda, Biashara ,Kilimo na Mifugo katika shamba la wakala wa mbegu kilimi nzega mkoani Tabora
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo ASA Dkt ,Sophia Kashenge akitoa maelezo juu ya teknolojia ya umwagiliaji kwa mwenyekiti na naibu wa ziri na wajumbe wa kamati ya ya kudumu ya bunge ya Viwanda, Biashara ,Kilimo na Mifugo inavyofanya kazi na hapo walipo juu ya kichanja inachovuta maji kupanda juu.
Mwenyetikiti wa kamati ya ya kudumu ya bunge ya Viwanda Biashara Kilimo na Mifugo Mariam Ditopile akitoka kwenye mbiundombinu ya umwangiliaji kwenye eneo la bwawa la kilimi wilayani nzega.
…..
Na Lucas Raphael,Tabora
Serikali imetakiwa kuendelea kulisaidia Shamba la Mbegu kilimi wilayani Nzega kuendelea kutumia teknolojia ya umwagiliaji ambayo ndio suluhisho pekee la kuchochea mapinduzi ya kiuchumi kwa kuongeza uzalishaji wa mbegu kutoka tani 200 hadi tani 3000 kwa mwaka.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyetikiti wa kamati ya ya kudumu ya bunge ya Viwanda Biashara Kilimo na Mifugo Mariam Ditopile mara baada ya kushuhudia uwekezaji mkubwa unaotekelezwa na serikali katika mradi wa umwagiliaji kwenye shamba la Kilimi kuzalisha Mbegu bora za kilimo lililopo wilayani Nzega mkoani Tabora
Alisema kuwa teknolojia ya umwagiliaji ndiyo njia pekee itakayoleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii hapa nchini kupitia sekta ya kilimo.
Mariam alisema kwamba serikali iendelea kuwekeza maeneo mengine kwa ajili ya upatikanaji wa mbegu bora za kilimo jambo ambalo litafanya bei ya mbegu kupungua tofauti na ilivyo sasa .
Alisema kwamba wizara ya kilimo iombe fedha kiasi chochote wanachotaka kwenye bajeti kuu ya serikali kwa ajili ya kuendelea na kuboresha teknolojia ya umwagiliaji .
“Kamati ya bunge kauli mmoja tunapongeza kazi nzuri unayofanywa na wakala wa mbegu nchini Asa kupitia mtendaji mkuu wa ASA kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuhakikisha fedha zilizitolewa na serikali zinafanya utekelezaji uliobora na wenye tija” alisema Ditopile.
Alisema kwamba kupitia teknolojia ya umwagiliaji uzalishaji wa mbegu utaongezeka kutoka tani 200 kwa mwaka 2022 hadi kufikia tani 3000 kwa mwaka 2024 utasaidia kupunguza kiasi kikubwa cha mahitaji ya mbegu nchini .
Awali Naibu Waziri wa Kilimo Davidi Silinde aliambaia kamati hiyo kwamba serikali inaendelea na jitiada za kuboresha mashamba ya wakala wa mbegu kwa kuwapatia fedha na kwa ajili ya utekelezaji wa teknolojia ya umwagiliaji ili kuweza kuzalisha mbegu kwa kipindi chote cha mwaka .
Alisema kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha nchi inazalisha mbegu nyingi na hilo linasababishwa na kuangiza mbegu kutoka nje ya nchi kwani fedha nyingine za kigeni zinatumika kwa kazi hiyo .
Ndoto ya mheshimwa Rais ni kutumia mashamba yetu kupitia kwa wakala wa mbegu nchi ambao ni ASA kuzalisha mbegu bora na mfano mzuri ndio hapa kilimi ambapo utaona teknolojia ya umwagiliaji inafanya kazi ya uzalishaji wa mbegu“alisema Naibu wa waziri Silinde
Hata hivyo alisisitiza kwamba kazi ya kuzalisha mbegu sio serikali pekee yake itafanya kuwaalika watu na Sekta binafsi kuja kuja kuungana nasi.
Nainu waziri aliwatoa hofu wadau wazalishaji wa mbegu kujitokeza kupata elimu na maelekezo ili kuungana kwa pamoja kwa ajili ya kuzalisha mbegu zilizokuwa bora za kilimo,
Shamba la mbegu la Kilimi uzalisha mbegu za Alizeti, Choroko ,Mahindi na Mtama na kuzisambaza katika ukanda wa magharibi na ziwa.